Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la benki ya TPB Mto wa Mbu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Profesa Lettice Rutashobya. Uzinduzi wa tawi hilo la Mto wa Mbu ulifanyika jana huko Mto wa Mbu, Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa benki ya TPB Ignas Mkawe, mara baada ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo hulo Mto wa Mbu, Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Simbamwene kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, Mkoani Arusha.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja, Ester Mfuru, wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, wakati wa uzinduzi wa tawi hili. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof. Lettice Rutashobya.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Bank Profesa Lettice Rutashobya, akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililopo Mto wa Mbu Arusha. Akitazama ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya TPB Mhe. Dkt. Philip Mpango (c) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. Kutoka kulia waliokaa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshigi na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Lettice Rutashaobya. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Waliosimama nyuma ni baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Benki ya TPB mara baada ya kuwasili kwenye tawi la Benki hiyo , tayari kwa kulizindua. Kulia na Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya TPB, Sabasaba Moshingi
Benki ya TPB imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Lengo la kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.
Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki yao.Alisema pia wananchi wa Arusha, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.
‘Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.
Alisema kwa sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini.‘TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, mwazoni mwa mwaka jana tulifungua matawi katika Mkoa wa Ruvuma, Kilimanjaro na Babati mkoani Manyara,’ alisema.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango alisema serikali itakuwa bega kwa bega na TPB kutokana na jitihada zake za kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na hata mawakala.
‘Mimi binafsi na serikali tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha taasisi za kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa katika shughuli za kiuchumi nchini, ikiwemo kuwawezesha wazalishaji kuboresha ufanisi na tija kwa mambo ya msingi katika ukuaji wa uchumi,’ alisema.
Alisema pia serikali itaendelea kutoa msukumo kwa sekta za kibenki pamoja na zingine juu ya umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na utoaji wa huduma kwa kuamini kwamba teknolojia bora huwezesha kuboresha ufanisi, kupunguza gharama na kupanua wigo wa soko.Naye Meneja wa TPB tawi la Mto wa Mbu, Selestine Mteta alizitaka taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment