Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Ltd. (Ensol) wamezindua mfumo wa umeme wa nishati ya jua katika kijiji cha Mpale kilichopo wilaya ya Korogwe, na hivyo kuwezesha umeme katika eneo hilo kwa mara ya kwanza. Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk. Juliana Pallangyo ambaye aliipongeza kampuni ya Ensol na washirika wake ikiwemo UNCDF kwa juhudi zake kubwa za ushawishi wa umeme hasa umeme mbadala wa jua ili kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa. Dk. Pallangyo alisema kwamba serikali ya Tanzania inawashukuru watu wa Ensol kwa juhudi zao kubwa za kupeleka umeme vijijini. Alisema kwa Ensol kuweza kufikisha umeme katika maeneo ya ndani kabisa ya kijiji cha Mpale, kuwaunganisha wananchi na umeme wa saa 24 na wamefanikiwa kubadili maisha ya wananchi hao.

No comments:
Post a Comment