Michezo :StarTimes yazindua msimu wa tatu wa uoneshwaji wa ligi ya Bundesliga 2017/2018 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Aug 2017

Michezo :StarTimes yazindua msimu wa tatu wa uoneshwaji wa ligi ya Bundesliga 2017/2018






Na Agness Francis, Blogu ya jamii.


Kampuni ya Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya Bundesliga mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia vipindi vya startimes kwa wapenzi wa soka hapa nchini


Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa kuwafahamisha wapenzi wa mpira kununua ving’amuzi na kujiunga na vifurushi ili kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa moja na startimes.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo kufanya mashindano ya uandishi wa mechi hiyo na kwa mshindi wa shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege kwenda moja kwa moja Ujerumani.


Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema wana mahusiano mazuri na bundesliga kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.


Meneja Uwendeshaji Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa huduma mpya ya malipo kwa wale wenye hali ya chini wanaweza kulipia siku moja king’amuzi cha Startimes kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.


Hata hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema kuwa ligi ya Bundesliga ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na ligi zingine duniani kwa kuwa na wachezaji bora


Nae Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa kampuni ya startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe 18-27 Agosti mwaka huu

Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini.


Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo

Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports Bar', Shaffih Dauda akitoa uchambuzi pamoja na kubashiri ligi hiyo itakavyokuwa kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.

Mhariri mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi wa kuonesha ligi hiyo kwa mwaka wa tatu kupitia kwenye king’amuzi cha Startames.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga


Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad