Matukio : Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akagua Miradi Wilaya ya Mbeya Mjini - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


1 Aug 2017

Matukio : Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akagua Miradi Wilaya ya Mbeya Mjini










Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa (wanne kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017. Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa (kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maua kutoka kwa mtoto , Felista (4) wa Shule ya Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS – PEPSI kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wa Shule Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad