Matukio: Wadau Wahamasishwa Kusaidia Ushiriki wa Tanzania Tamasha la JAMAFEST - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 19 August 2017

Matukio: Wadau Wahamasishwa Kusaidia Ushiriki wa Tanzania Tamasha la JAMAFEST



Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akikiwasilisha mada katika mkutano wa wadau katika kuchangia ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi akizungumza kwa niaba ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano wa wadau katika kuchangia ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group (CMG), Bw. Ruge Mutahaba akichangia mada wakati wa kikao cha wanakamati ya maandalizi ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Bw. Nelson Madirisha akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau kufanyikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Picha ikionyesha namba zinazotumika kupokea michango kutoka kwa wadau kwa ajili ya kusaidia ushiriki wa wasanii kutoka Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) itakayofanyika Jijini Kampala Uganda mapema mwezi Septemba.

Mmoja wa wadau wa Sanaa na Utamaduni Bi. Esther Baruti akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau kufanyikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Mmoja wa wadau wa Sanaa na Utamaduni akijaza fomu baada ya kutoa ahadi ya kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, katika mkutano uliowakutanisha wanakamati walioteuliwa na Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

Baadhi ya wadau waliofika kwenye mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi ili kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, katika mkutano uliowakutanisha wanakamati walioteuliwa na Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

No comments:

Post a Comment