Na David John Mwanza
JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanatumia kalamu zao kwa uweledi na uadilifu mkubwa katika kuhabarisha umma, mambo muhimu ya nchi na kwamba waepuke kutumiwa na watu wachache ambao mara zote hawalitakii mema Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Rpc Mohamed Msangi wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ambaye aliongozana na Naibu katibu kuu wa Taasisi ya kutetea haki za binadamu nchini TAHURA Habibu Rajabu jana.
Kamanda Msangi mbali na mambo mengine alisema kuwa waandishi wa habari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa salama kwani kama kalamu zao zitatumika vibaya ni rahisi kuvunja usalama ambao umejengwa na waasisi wa Taifa.
"Nitowe wito kwa waandishi wa habari ni vema wakaongeza uzalendo na uchungu kwa nchi yao na hasa kuhakikisha mnatumia kalamu zenu kwa ustadi wa hali ya juu na kuepuka kutumiwa na watu ambao hawalitakii mema taifa,".alisema Msangi
Aliongeza kuwa katika suala la kulinda amani linatakiwa kwa kila mtanzania, kwani hata mwandishi wa habari ni mtanzania na pindi usalama utakapokosekana haitajalisha nafasi ya mtu hivyo lazima waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wazalendo la kuhakikisha wanapigania taifa lao kwa nguvu zote.
Msangi alifafanua kuwa watanzania wasidanganywe kwani uhuru ambao unapatikana hapa nchini huwezi kupata mahala pengine popote hivyo ni lazima kujiepusha na watu ambao wanataka kujipatia umaalufu kwa mgono wa watu wengine wakiwemo wandishi wa habari.
Akizungumzia hali ya usalama katika mkoa wa mwanza Kamanda Msangi alisema jiji hilo lipo salama na watu wanaendelea na shughuli zao kama ilivyo maeneo mengine huku akikiri kuwepo kwa matukio madpmadogo ambayo kimsingi jeshi la Polisi linaendelea na uperesheni zake za kila siku.
"Mwanza iki shwari na hata ninyi wenyewe mnaona kama watu wanaendelea na kazi zao japo matukio madogo madogo hayakosekani hususani uwizi wa pikipiki na kadhalika lakini askari wangu wako wanaendelea na majukumu yab kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa salama."alisema Msangi.
Pia aliwataka wananchi wa mwanza ma tanzania kila mtu kujitambua na zaidi kuhakikisha kauli ya viwanda wanaipiokea kwa kufanya kazi huku akibainisha wao kama mkoa wameshatenda maeneo kwa ajili ya kukaribisha uwekezaji kwa manufaa ya nchi huku akisisitiza kwa kuzitaka taasisi za haki za binadamu kuwa makini kupokea malalamiko ya watu pasipo kuyachunguza kwa kina.
"Nivema taaisis za zinateteta haki za binadamu kufanya kazi zao kwa uweledi na kuhakikisha malalamiko wanayoletewa wanayafanyia kazi kabla ya kuchukua hatua ambazo mwisho wa siku zinaleta madhara kwa wananchi husika.alisema Msangi.
Ambapo kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa Tahura Habibu Rajabu aliunga mkono kauli ya RPC Msangi huku akishauri kwamba wananchi wajitahidi kuleta malalamiko kwa wakati na si kusubiri muda mwingi umepita lakini hata wakileta ukifanya uchunguzi kwa kina unakuta alalamiko mengi ni yakweli lakini mengine ni siasa tu.
No comments:
Post a Comment