Matukio : RC Rukwa Amezionya Halmashauri Dhidi ya Matumizi Mabovu ya Mashine za EFDs - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Aug 2017

Matukio : RC Rukwa Amezionya Halmashauri Dhidi ya Matumizi Mabovu ya Mashine za EFDs



RC Rukwa Mh. Zelote Stephen akiwaonesha waheshimiwa madiwani (hawapo pichani)risiti ambazo tayari zimeshakatwa kabla ya kutumiwa.

RC Rukwa akiwaonesha waheshimiwa madiwani (hawapo pichani) kitabu cha hoja za mthibiti na mkaguzi wa serikali kwa Manispaa ya Sumbawanga.

RC Rukwa akitoa ufafanuzi.
…………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine za EFD kwa kuongeza mapato katika halmashauri zao.


Ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili hoja hizo zisijirudie miaka inayofuata.
Akiongea huku akionesha risiti alizozikamata katika maeneo mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali inafanya kila liwezalo katika kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado kuna watumishi wanatafuta namna ya kuiskosesha serikali mapato hayo.


“katika kila sehemu za mauzo lazima mashine hizi ziwepo na kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu wa risiti zilizokatwa tayari kwa matumizi) hizi nimezikamata maeneo anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana, ndio mchezo uliopo, pamoja na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu za kuiba, hii sio kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu kuwa mimi ni mtaalamu wa kukamata,”Alisema


Katika Kusisitiza suala la uwazi wa matumizi ya fedha za halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote alitaja majukumu kadhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja ya kazi za Mkurugenzi ni kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halmashauri.
“Hapa mmezungumza na mmenionyesha kwa kiasi kikubwa kwamba hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo ya waheshimkwa madiwani ni kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna taarifa,” Alisema.


Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio katibu wa kamati ya fedha ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati hiyo ibebe sura ya halmashauri na sio sura ya kamati na kuwasisitiza kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha mrejesho kwa wengine juu ya mipango na maazimio yaliyofikiwa.
Katika kikao hicho Mh. Zelote alimtambulisha mtaalamu wa TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani namna mifumo ya fedha inavyofanya kazi ili nao wawe na uelewa mpana katika kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri.



“Suala la kukusanya mapato limekuwa likiimbwa asubuhi, mchana na usiku, kuwa tuhakikishe tunajipanga vyema kukusanya mapato ya halmashauri kwa kupitia utaratibu uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la kuhoji tena mwisho ulikuwa mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi kuwa mashine hizi ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema.


Na katika kuhakikisha kuwa vitabu hivyo havipati nafasi Mh. Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa watumishi wanaokiuka miiko ya kazi zao kuwajibishwa kulingana na madhara waliyosababisha na kuwaasa kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya halmashauri.


“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye mkoa wangu kuna halmashauri inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole mara moja sitaki kuona tena hicho kidole,” alimalizia.


Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya nSumbawanga Mh. Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao kushindwa kudhiti hoja na hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha hoja.


“Mtu kama unaitwa mtaalamu na serikali imekuamini kwanini tena unaizalishia serikali hoja, na suala la fedha ni suala nyeti sana hivyo linahitaji umakini wa haloi ya juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili na si vinguinevyo,” Alisema.


Akifunga kikao hicho Mstahiki meya wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yale yote aliyoyaelekeza na kuomba msaada wake pindi pale watakapokwama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad