Katibu Tawala wa Mkoa wa Dododma Rehema Madenge akifungua mafunzo ya siku nane kwa wataalamu wa Afya, Mipango na Fedha kutoka Mikoa Mitano chini ya ufadhili wa mradi wa Uimarishaji Mifumo (PS3)
SERIKALI kuanzia sasa inaweza kuokoa zaidi ya Sh Bilioni tisa ambazo zilikuwa zikutumiwa na maofisa wake mbalimbali katika uandaaji wa mipango na bajeti katika Serikali za mitaa na Halmashauri kufuatia kuanza kwa matumizi ya mfumo mpya wa uandaaji mipango na bajeti utakaotekelezwa chini ya mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3). Anaandika Mroki Mroki wa DAILY NEWS Digital.
Mradi wa PF3 unatekelezwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa watazindua Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep), Mratibu wa Mfunzo hayo, ambaye pia ni Mtaalaam wa Mifumo ya Tehama na Mawasiliano kutoka PS3, Desderi Wengaa, alisema katika mfumo wa zamani uliokuwa unatumika ulikuwa ukiwafanya watendaji wa serikali kutumia muda mrefu na gharama kubwa kuandaa mipango na bajeti zao lakini huu wa sasa utaokoa muda na gharama ambazo zinazidi bilioni tisa kila mwaka.
“Mradi huu kupitia mfumo wa PlanRep utasaidia san asana kuokoa gharama kwaa maana ya rasiliamali fedha zilizokuwa zinatumiwa na serikali takribani Sh milioni 60 kwa kila halmashauri na zaidi ya Sh bilioni nane hadi tisa au kumi kwa nchi nzima kwa kutumia mfumo huu ambao pia utawawezesha watendaji kufanya kazi za kutoa huduma katika maeneo yao badala ya kuzunguka katika vikao vya kuandaa bajeti,” alisema Wengaa.
Washiriki wa Mafunzo hayo ya namna ya kutumia Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep),wakifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa mradi pamoja na mgeni rasmi ambaye alikwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.

Mwakilishi wa washiriki wa Mafunzo hayo, Dk Aisha Mahita akitoa neno la Shukrani kwaniaba ya washiriki wote.
Miongoni mwa wakufunzi wa mafunzo hayo ni timu ya kitaifa ya wakufunzi kutoka TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa, Wakala ya Serikali Mtandao (Ega), Ofisi ya Raisi Menejimenti na Utumishi wa Umma, Wizara ya Fedha na Mipango, PS3 pamoja na wizara zingine ikiwemo Wizara ya Afya.
Zaidi ya watumiaji 1,500 watafundishwa juu ya mfumo wakiwakilisha ngazi tatu za Serikali. Mafunzo haya yanajumuisha Maafisa Mipango, Wahasibu, Wachumi, Maafisa Tehama na Makatibu wa Afya wa Halmashauri.
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.
Washiriki wa Mafunzo hayo ya namna ya kutumia Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep),wakifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa mradi pamoja na mgeni rasmi ambaye alikwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.
Meza kuu katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment