Mapishi na Chef Kile : Jinsi ya Kupika Njegere Nazi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Aug 2017

Mapishi na Chef Kile : Jinsi ya Kupika Njegere Nazi

Tangu nilipokuwa mdogo ilikuwa siku wakipika njegere na tukala na wali kusema kweli nilikuwa nafurahi kiwango kikubwa sana. Zaidi pale inapokuwa njegere zimeungwa na tuzi zito la nazi. Sasa nishakuwa mtu mzima na najua kupika hivyo mara nyingi huwa najipikia.

Hili ni pishi moja rahisi sana kwa yeyote anaweza pika bila kukosea. Mahitaji ya kawaida tu ni njegere, nazi, vitunguu , nyaya ila sasa kuna ziada ili kuongeza nakshi nakshi na ndio mimi sasa leo nakuelekeza vile ambavyo mimi huwa napika

MAHITAJI
Glass 3 za njegere
Vitunguu maji viwili – vikatwekatwe
Nyanya 3 – Zimenywe na kukatwa katwa
Karoti moja – Ikatwe vipande vidogo dogo
Mchanganyiko wa Kitunguu swaumu na Tangawizi kijiko 1 cha chai
Mahanjumati masala kijiko 1 cha chai – Waweza tumia spice mix aina yoyote ikiwa hauna Mahanjumati masala
Tui zito la nazi Glass moja 1
Mafuta ya kula vijiko 3 vya mezani

JINSI YA KUPIKA
Kwanza chemsha njegere zako hadi kuiva ila sio kurojeka – zikiwa tayari weka kando
Weka chombo unachotumia kuunga mboga na uweke mafuta yakiaanza kupata moto weka vitunguu maji na endelea kukaanga hadi vilainike
Vikiisha kulainika weka ule mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi. Endelea kuvipika vikiwa kama vinaanza kubadiri rangi sasa weka zile nyanya.
Zipike nyanya hadi zitakapoiva na kuwa kama zinatengana na mafuta ndipo unaweka karoti na mahanjumati masala au spice mix ulionayo kwa sekunde chache kisha unaweka njegere
Ili zisiwe kavu sana unaweza ongeza kidogo yale maji yaliyotumika kuchemsha njegere. Ongeza na chumvi kiasi upendacho. Kisha mchanganyiko huo uendelee kuchemka kwa dakika 3-4
Sasa weka lile tui la nazi na punguza moto. Baada ya kuweka tui la nazi endelea kukoroga kwa dakika chache hadi itakapoanza kuchemka taratibu. Baada ya hapo epua na tayari kwa kula.

Furahia pishi hili zuri la Njegere Nazi. Hapa chini nimeweka video nikionyesha jinsi ya kukuna nazi na kutengeneza tui la nazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad