Kilimo Kwanza : Simbachawene ahamasisha Teknolojia ya Kilimo Ihamishiwe kwa Wakulima - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Aug 2017

Kilimo Kwanza : Simbachawene ahamasisha Teknolojia ya Kilimo Ihamishiwe kwa Wakulima



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(kulia)akipewa maelezo ya namna ya kulima bila kutumia udongo na Mtalaamu wa kilimo wa kampuni ya Rijk Zwaan alipotembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu hiyo kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akiangalia namna kikundi cha Nronga Women Dairy cha wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinavyojishughulisha na uuzaji wa maziwa kwenye banda la halmashauri ya Hai kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Hai,Gelasius Byakanwa.

Nteghenjwa Hosseah - Arusha
Nane nane ni miongoni mwa maonyesho maarufu Nchini Tanzania ambayo huwagusa na kuwakutanisha wakulima, wafugaji, wavuvi wa Mjini na Vijijini, Taasisi za Serikali na binafsi zinahusika na sekta hiyo zilizopo ndani na nje ya Nchi pamoja na Wadau wa Kilimo.

Maonyesho ya Nane nane hutoa fursa kwa wadau wote wa sekta ya Kilimo kuonyesha bidhaa mbalimbali za Kilimo, kuuza bidhaa hizo, kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia mbalimbali zia kuboresha Sekta ya Kilimo ili kuondokana na Kilimo cha kufa na kupona na kuwa Kilimo chenye Tija kinanachofaa kwa biashara na kutosheleza kwa chakula.

Katika historia ya maonyesho haya ambayo wakulima kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini hushiriki ili kujifunza teknolojia hizo mpya za Kilimo kumekuwa na mabadiliko kidogo katika eneo la utekelezaji wa Teknolojia hizo katika maeneo yao.

Huenda tatizo likawa ni uelewa mdogo wa wakulima wetu wanaoshiriki katika maonyesho hayo, kutokujifunza kwa umakini kuhusu mbinu hizo za kisasa au kukosekana kwa uwezeshaji wa wananchi katika kutekeleza mbinu hizo kwenye maeneo yao au kutokuwa na usimamiza wa maafisa Ugani katika maeneo mengi ya Kilimo Nchini.

Ushiriki wa mazoea katika Maonyesho haya unaelekea kufika mwisho baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kufungua Maonyesho ya 24 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyiika Mkoani Arusha katika viwanja wa Themi – Njiro.

Wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho hayo Waziri Simbachawene alikagua mabanda mbalimbali ya Kili mo na Mifugo ya Halmashauri za Kanda ya Kaskazini, Sekta binafsi za Kuzalisha Mbegu bora, Pembejeo, Zana za Kilimo viwatilifu pamoja na dawa za Mifugo na kujionea teknolojia bora na za kisasa zinazoweza kumsaidia Mkulima na Mfugaji kuachana na kilimo cha kujitaftia chakula na kuhamia kwenye biashara njia itakayoweza kumuo ngezea kipato na kumwinua kiuchumi.

Akifungua Maonyesho hayo Mhe. Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauro zote Nchini sambamba na Maafisa Ugani kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye maonyesho haya na kwenda kuwafundisha wananchi na kuwawezesha kuzitekeleza katika maeneo hayo.

Amesema kuanzia mwaka huu nataka maonyesho haya yanalete mabadiliko kwa wananchi wetu kwa kuwawezesha kulima kwa Tija kwa kutumia eneo dogo na kuweza kupata mazao mengi, kufunga kisasa kwa kuwa na mifugo bora na michache lakini yenye faida kubwa pamoja na kuanzisha ufugaji bora wa samaki katika maeneo mengi Nchini.

“Kuanzia mwakani tutaanza kufanya tathmini ya namna ambavyo maonyesho haya yamebadilisha maisha ya wakulima wetu katika Halmashauri na sio kila mwaka Halmashauri zinashiriki lakini hamuondoki na kitu kipya wala hamuwasaidii wakulima wa kule vijijini ambao huenda hawapati fursa ya kuja kuona mapinduzi haya katika Kilimo”.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho haya Kanda ya Kaskazini amesema katika mara hii ya kwanza ambapo maonyesho haya yametoka kwenye Chama cha Wakulima na Wafugaji (TASO) na kuratibiwa na Serikali wamejitahidi kushirikisha wadau mbalimbali wenye teknolojia tofauti tofauti ili kuweza kutoa wigo mpana kwa wakulima na wafugaji kujifunza zaidi.

Pia aliongeza kuwa ameunda kamati ambayo itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro kuchunguza namna ambavyo TASO walivyokuwa wanafanya kazi, Mali zinazomilikiwa na Taso, Mapato yaliyopatikana wakati wa uratibu wao na namna ambavyo yalitumika na mgawanyo wa kazi zao na kuja na usahuri wa kitaalam juu ya nini kifanyike katika kuboresha zaidi usimamizi wa maonyesho hayo.


Waziri Simbachawene amefungua maonyesho haya ikiwa ni ya Pili tangu maadhimisho ya Sherehe hizi yalipoanza na alifungua Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo – Lindi na atafunga maoneysho katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad