Jeshi /Afya : JKT Mgulani Yachangia Damu Hospitali ya Rufaa ya Temeke na Kufanya Usafi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 31 August 2017

demo-image

Jeshi /Afya : JKT Mgulani Yachangia Damu Hospitali ya Rufaa ya Temeke na Kufanya Usafi


1
Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote.
IMG_3662
Jengo la Utawala la Hospitali hiyo.
IMG_3663
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Bilal Babu akimtoa damu, Kijana wa JKT, Damiani Ambross wakati akichangia damu.
IMG_3667
Vijana wa JKT, wakisubiri kuchangia damu.
IMG_3680
Vijana wa JKT wakisukuma mkokoteni wenye matofari wakati wakifanya usafi katika hospitali hiyo.
IMG_3684
Vijana wa JKT wakiweka matofari katika eneo maalumu
IMG_3686
Usafi ukiendelea kufanywa.
IMG_3688
Mti ukikatwa.
IMG_3699
Matawi ya mti yakikatwa tayari kwa kuondolewa
IMG_3704
Usafi ukiendelea.
IMG_3715
Hapa ni kazi tu ya usafi.
IMG_3716
Mti uliokatwa ukisukumwa tayari kwa kuondolewa katika eneo hilo.
IMG_3718
Mti uliokatwa ukiondolewa eneo la tukio.
IMG_3725
Askari hao wa JKT wakiondoa matawi ya mti yaliyokatwa.
IMG_3726
Takataka zikiondolewa hospitali hapo kwa kutumia mifuko maalumu.
IMG_3729
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Hassan Mwage akimtoa damu, Kijana wa JKT, Kafumu Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
IMG_3730
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Heri Shekighenda akimtoa damu, Kijana wa JKT, Kafumu Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
IMG_3734
Vijana wa JKT wakijisajili majina yao kabla ya kutoa damu kwaajili ya kuchangia.
IMG_3737
Takataka zikiondolewa.


Na Dotto Mwaibale

ASKARI wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi namba 831 KJ Mgulani, wamejitolea kuchangia damu pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Zacharia Godfrey Kitani alisema kila maadhimisho hayo yanapofanyika wamekuwa wakifanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi na mwaka huu wameona wafanye usafi na kuchangia damu katika hospitali hiyo ili kusaidia wananchi.

"Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maerneo tofauti tofauti kwa siku kadhaa leo hii tunafanya usafi katika Hospitali ya Temeke na kutoa damu na tutaendelea katika maeneo mengine hadi siku ya kilele cha maadhimisho haya hapo kesho kutwa" alisema Kitani.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Husna Msangi alisema msaada huo wa damu waliochangia askari hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.

Alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha kwa kukosa damu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *