![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMB3QwXT4VNyev9CybMPeisYu2hG29CP5gXqUF5Qq1HO7K_Cq8JOBP7OyzZn4-HucFUgabBxd3roUnNFwvSLPnc72P-FQcC-1A3VR8cHK9YhtWuS8je8-5_8IgAGiN8AZRlUlfcIRy6y8/s640/172085_197470153600339_170549112959110_833407_8067131_o%25283%2529.jpg)
Sekta ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka huu wa fedha.
Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa maendeleo ya watanzania wote.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRxYP3L-6dg3Eh2gGJjQlWNCDXrU62IzCvD5e6anc_-gW-HKWGIRMRdxCOs9BVDKdBaTc145Fn1TCYYDEYWcmPAUtMRd2s-fwJA4MHIfQihKQSua-N8U4o_Je9MTXIz8dYjF8JugcYFLA/s640/lake-chala3.jpg)
Aliongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrnlzJNDbjM4cmAPXGQemN3zAYGBJUDDRYbPUrlDWcyTRaNQiokFSB9ydlUaUvGbA3PMQnAD6JkqSFHYruD88nwHnyT4Z08DoMhQ5psL-GVIl4me680p-4h69NHlrjBYRdtAYxBDZAqLs/s320/static1.squarespace.com.jpg)
Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri, hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini ndiyo sababu zinazowavutia watalii kuongezeka kila mwaka.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinaU0woxlTeZ-zw3sx58DrLqV3jHqypTAcXLOoZ7ULWsYNTnAN4USnShEP43BefQPNoCYBO2iPVNIs5iK7PqjJV2x2rnMnSkPio0vh89Xk0jOUoHY9K-4jyCGoEBaP14yM3SQ-3Cwvq1U/s640/zanzibar-91_high.jpg)
Hivi karibuni Mtandao wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii barani Afrika uliitaja Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za watalii barani humu.
No comments:
Post a Comment