TANZIA : Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Shebuge Afariki Dunia - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 7 July 2017

TANZIA : Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Shebuge Afariki Dunia




Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.






Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagara Majimatutu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.






Kwa mujibu wa taarifa ya kitaama iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.






Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.






Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.






IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA



No comments:

Post a Comment