Matukio : Waziri, Lukuvi Awezesha Ujenzi wa Mabweni, Iringa - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Jul 2017

Matukio : Waziri, Lukuvi Awezesha Ujenzi wa Mabweni, Iringa



Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa ndani.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Eneo la kunawia lililo ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.

………………………….

Na Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ismani Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan amesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi Iringa Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.

Ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali la shule hiyo kuteketea kwa Moto.

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

“waziri Lukuvi lileta maombi ya miradi mbalimbali ambayo miongoni mwake ni kujengewa Hostel ya wasichana ya shule ya Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka 2008, kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa, kwa hiyo namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo”

“Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji wa Hosteli hii umekamilika ikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi, na ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema”

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo.

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri.

Waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine amewataka wanafunzi hao kutunza mabweni hayo na kujiepusha na hatari zozote za kuchoma moto, kitendo ambacho kinasababisha upotevu mkubwa wa mali na uhai wa wanafunzi hao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad