Na Freddy Macha Kutoka London : Balozi Dk. Asha-Rose Migiro akutana na Watanzania Waishio London - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Jun 2017

Na Freddy Macha Kutoka London : Balozi Dk. Asha-Rose Migiro akutana na Watanzania Waishio London

Na Freddy Macha,London

 Kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ubalozi wa Tanzania huchagua usiku mmoja ambapo wananchi wa madhehebu yote hualikwa kufuturu. Jumamosi 10 Juni, 2017 shughuli hii haikufanywa Ubalozini, wala haikuwa ya bure. Washiriki tulitakiwa kuchangia pauni 10 (kama shilingi 25,000) kutopoteza kodi za wananchi nje. Si kiasi kikubwa na kina mama nao walijitolea kupika na mikeka kukalia. Pili, mkutano wa takriban saa 3 na nusu uliwakutanisha Watanzania na Balozi Asha Rose Migiro kutathmini mada mbali mbali muhimu kabla ya kula. Desturi hii ni ya kipekee kwa Watanzania na sijawahi kusikia ikifanywa na mataifa mengine. Zingatia pia kuwa kikao kilifanywa kanisa la Monravia, Hornsey kaskazini ya London.

Balozi Migiro, akiwa na mtangazaji marufu mstaafu wa Redio, Chama Omari Matata. Enzi zake, Bw Matata alitisha. Ni hazina ya taifa. Alisifika na kujulikana sana miaka ya 1960, 70 na 80, Radio Tanzania na baadaye Idhaa ya Kiswahili BBC, London. Mwakilishi wa mkutano wa Albino , unaofanyika London 12 na 13 Juni, kuadhimisha siku ya kimataifa ya Albino 2017, Josephat Torner, akiwaeleza waliokuwepo, kifupi, juu ya harakati hizi za kinyama. Saidi Surur akimkaribisha Mheshimiwa Balozi kuongea na wananchi Muambata Jeshi Ubalozini, Kanali Jackson Mwaseba, na Mwakilishi wa Albino Tanzania, Josephat Torner baada ya mkutano. Mtanzania Joseph Keyo akitoa hoja na kuuliza swali Bi Patricia Mpangala akizungumzia namna vijana wengi wa Kitanzania wanavyoendelea kujazana jela za Uingereza kutokana na ukosefu wa msimamo imara Bi Zuweina Kayugwa akielezea umuhimu wa kufundisha Kiswahili kwa watoto waliozaliwa Ughaibuni. Balozi Migiro alizungumza takribani saa tatu bila kuonesha uchovu Simon Mzuwanda akisaili kuhusu umiliki wa ardhi na uraia pacha Doris Mawala, mkazi miongo mingi London, akisisitiza haja ya Watanzania kujuana na kukutana mara kwa mara. Tabia hii imefifia siku hizi, alidai. Baadhi ya maakuli Picha ya pamoja Balozi Migiro na vijana wanaosoma Uingereza Mheshimiwa Balozi akizungumza na baadhi ya kina mama wengi waliojumuika kwa kuchangia hoja, kupika, nk Simon Mzuwanda , Tunu Baraka, na Dora Mawala wakiwa na Mwakilishi wa kimataifa wa Unyanyasaji wa Albino Tanzania, Josephat Torner(wa tatu toka kushoto). Bi Dola Songambele, alizungumza kwa hamasa kuhusu udhaifu wa kuungana Watanzania London. Kujua zaidi -Pitia “Kwa Simu Toka London” https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ

Post Top Ad