Maisha : Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Jun 2017

Maisha : Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji



Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho


Wakazi wa Kijiji cha Ngulu kitongochi cha Mkongea wilaya ya Mwanga wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu bila kutatuliwa hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika. Mkazi wa kijiji hicho, Halima Miraji alisema kuwa tangu mwaka 2004 wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo kwa muda mrefu sasa maji yamekuwa yakitoka usiku wa manane tu.

Halima alisema kuwa mfumo wa maji ulijengwa kwenye kijiji jirani cha Mgagani mwaka 1992 ambapo vijiji vyote viwili vilikuwa vikipata maji kutokea hapo. Hata hivyo, alisema wakati wa mafuriko, miundombinu iliharibika na hivyo kusababisha maji yapungue na ndipo viongozi wa vijiji hivyo viwili walipoamua kuwa maji yawe yanafunguliwa kwenye kijiji cha Ngulu nyakati ya mchana na kijiji cha Ngulu wakati wa usiku.

“Kutokana na changamoto hiyo, wanawake tunalazimika kuamka usiku wa manane kuchota maji kwa kuwa kwa kawaida huwa yanakatika alfajiri,” alisema Halima. Alisema kwa kuwa wanawake ndio wanaochota maji usiku na badhi ya wanaume wachache ambao hawajaoa, kutokana na hilo alisema kuwa badhi ya wanawake walijikuta wakiianza uhusiano na wanaume jambo ambalo limefanya ndoa zao kuvunjika.

Alisema kila mtu hulazimika kuweka ndo moja kwenye foleni ya maji iliyo na watu Zaidi ya hamsini kabla ya mzunguko kurudia mara ya pili, tatu na kadhalika jambo ambalo liliwafanya badhi ya wanawake kuingia kwenye vishawishi wakati wanasubiri kwenye foleni. Alisema kuwa changamoto nyingine, ni kuwa shughuli nyingi kama kilimo, biashara na kutunza familia zimekuwa zikizorota kwa kuwa wanakuwa wamechoka asubuhi baada ya kuchota bmaji usiku kucha.

Mkazi huyo aliyasema hayo wakati Kituo cha tafiti Twaweza ilipokuwa kwenye zoezi la kujifunza hali halisi vijijini (immersion) ambapo wafanyakazi wake wote waliweza kuishi kwa siku tatu na familia za vijiji vya Ngulu kata ya Mwanga. Katika zoezi hili walibaini kuwa kukaa pamoja na jamii huwaleta karibu na hivyo husaidia kueleza changamoto zao zinazowakabili kila siku ambazo zimekuwa kikwazo cha maendeleo.

Kutokana na hilo, Twaweza waliweza kugundua changamoto nyingi, ikiwemo, kwenye sekta ya afya, elimu, maji na kadhalika ambazo zinahitaji ufumbuzi wa haraka. Kutokana na hilo wakazi wa Mwanga walishauri serikali kuhakikisha inakuwa karibu na wananchi wake ikiwezekana kutenga muda wa kuishi kwenye vijiji hivyo ilikuweza kutambua moja kwa moja kero zao na jinsi ya kuzitatua.

Wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza, Aidan Eyakuze, wafanyakazi wote wa Twaweza wakiwemo wale wa Tanzania, Kenya na Uganda walifunga ofisi na kwenda kwenye vijiji mbali mbali vya mwanga kujifunza hali halisi ya wakazi wa vijijini. Katika mwendelezo huo, mwenyekiti wa Kijiji cha Ngulu Modest Severine alisema kuwa tatizo la maji limekuwa sugu katika kijiji hicho na kuwa weka wakina mama katika wakati mgumu.

Alisema mradi wa maji ulipelekwa kwenye wnwo hilo mwaka 1992 lakini kisima kilijengwa kwenye kijiji cha Mgagao kwa makubaliano kuwa maji hayo yengetumika na wakati wa Mgagao pamoja na Ngulu. “Baada ya mradi kuharibiwa na mafuriko na badhi ya miundombinu kubebwa na maji, viongozi walikubaliana kuwa wakazi wa Ngulu wafunguliwa maji saa nane usiku,” alisema.

Alisema kuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw Jumanne Maghembe alipewa tarifa na kuahidi kutatua suala hilo. Alisema kwa mujibu wa mbunge huyo kuna mradi mkubwa wa maji unaoitwa Maji ya Mungu uliokwenye hatua za awali ambao utakuwa unapeleka maji kwenye vijiji vya Ngulu, Mgagao na Pangani.

Wakati huo huo, mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ngulu, Kiende Athumani nae alisema kuwa kitongoji cha Mkongea kimekuwa kikikabiliwa na tatizo ya maji kwa muda mrefu. Alisema kutokana na changamoto za maji, wakazi wa …wamekuwa wakitumia maji kumwagia mazao yao jambo ambalo linasababisha maji kutoka kidogo nyakati za usiku.

Alisema kuwa serikali imetariwa kuwa kuna mradi wa maji ya Mungu ambayo ikikamilika itakuwa ikitoa maji kwenye vitongaji mbali mbali ikiwemo mkongea, Kavagala, Kivengere na Mabashara. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho alisema kuwa changamoto ya maji kwenye kijiji cha Ngulu unatafutiwa ufumbuzi.

Alisema mradi wa Maji ya Mungu ukikamilika utakuwa unasambaza maji kwenye wilaya ya Mwanga na Korogwe. “Wakandarasi wapo kwenye eneo la ujenzi, na tunategemea mradi awamu ya kwanza uwe umekamilika ifikapo mwaka 2018,” alisema.

Alisema mradi awamu ya kwanza ukikamilika utakuwa umetatua kero ya maji kwenye wilaya ya Mwanga na Same na hivyo kuhakikisha wakazi wa Kijiji cha Ngulu wana maji ya kutosha. Aliongea kuwa, mradi awamu ya pili utanza pindi awamu ya kwanza utakapokamilika na tatizo la maji litaisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad