Uchumi : Waziri, Dk. Mpango akutana na viongozi Waandamizi wa IMF na Balozi wa Hungary - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 May 2017

Uchumi : Waziri, Dk. Mpango akutana na viongozi Waandamizi wa IMF na Balozi wa Hungary


Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang ameahidi kufungua madirisha ya mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukuza uchumi.
Bw. Zhang aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Shirika la Fedha la Kimataifa limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na ipo juu ya wastani wa ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.


Ameishauri Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi katika ukuaji wa Uchumi ili uchumi huo uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na mfumo shirikishi wa kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema kuwa juhudi za Tanzania kwa sasa ni kuchochea ukuaji wa Kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija
“Umasikini haujatatuliwa kwa kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa mpaka sasa watu walio katika umasikini na ukosefu wa huduma za lazima ni takribani asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango
Kama nchi imeamua kwenda kwenye uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa mkazo ni upatikanaji wa umeme wa kutosha na wenye bei nafuu.
Amesema kuwa Serikali imefanya juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini bado kazi hiyo haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya usafirishaji ni changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa nchi ambao ni wazamani na umeharibika.
“Serikali imeamua kujenga Reli yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) ambayo ni ya gharama, na kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola Bilioni 7.6, lakini umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango


“Tayari tumeanza ujenzi wa reli hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa 200 kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri fedha zinavyo patikana” alifafanua Waziri Mpango.
Amesema kuwa, kumekuwa na tatizo la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati jambo linalofanya baadhi ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni vema Serikali ikaendelea kuangalia vipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ili iweze kuchochea uchumi.
“Suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa kuwa Sekta Binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi nyingi Duniani” Alishauri Bw. Mkwezalamba.
Ameishauri Tanzania kuendelea kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa ni moja ya eneo ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo chanya na ya haraka katika ukuaji wa Uchumi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo, Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kunakuwa na viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata ajira. Aidha tayari Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kupata elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa pili kulia) akieleza kuwa Tanzania inakua kwa kasi kiuchumi jambo ambalo linawavutia viongozi wengi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake, alipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiongoza Mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (mbele kulia) ambapo alisema mahitaji makubwa wa nchi ni maendeleo ya kilimo na upatikanaji wa nishati ya umeme ili viweze kuchochea uchumi wa viwanda. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba ( kulia) wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao uliohusu suala la Uchumi katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (watatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu hali ya uchumi katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (hayupo pichani) wakimuaga baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akielezea kuhusu ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) ambapo alisema itasaidia kuchochea maendeleo si tu kwa Tanzania bali na nchi jirani, wakati wa Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu nia ya Shirika hilo kufungua fursa zaidi za mikopo kwa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam


Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kushoto) akionesha nia ya nchi yake kuwa na ushirika wa maendeleo na Tanzania utakao wezesha nchi hizo mbili kunufaika kiuchumi kupitia Sekta mbalimbali za Maendeleo, wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akizungumza kuhusu fursa zilizopo za uwekezaji katika Nishati, Miundombinu, Kilimo wakati wa Mkutano kati yake na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kushoto), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipongezana na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kulia), baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao kuhusu uwekezaji wenye tija kwa pande zote mbili. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (wa pili kushoto), wakibadilishana mawazo na wajumbe wengine walihudhuria mkutano kati yao kuhusu uwekezaji wenye tija, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es alaam.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kushoto) wakiagana baada ya kumalizika mkutano kati yao ambapo Balozi huyo ameonesha nia ya nchi yake kuwekeza nchini. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha na Mipango

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad