Kilimo Kwanza : TADB, TAHA Wapanga Kusaidia sekta ya Mali mbichi na Matunda (Horticulture) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 May 2017

Kilimo Kwanza : TADB, TAHA Wapanga Kusaidia sekta ya Mali mbichi na Matunda (Horticulture)


Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi akieleza utayari wa TAHA wa kushirikiana na TADB katika kukwamua changamoto zinazoikabili sekta ya malimbichi na matunda nchini.
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.



Na Mwandishi Wetu, Arusha.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA) zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza tija kwa kilimo hicho.

Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na kilimo kwa ujumla nchini.

“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad