Habari : Mwenyekiti wa APC Azungumzia Sakata la Waandishi wa Habari Kukamatwa , Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 May 2017

Habari : Mwenyekiti wa APC Azungumzia Sakata la Waandishi wa Habari Kukamatwa , Arusha

Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari Mkoani Arusha Bw. Gwandu Akizungumza na Vyombo vya habari Jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu,

Leo Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia mkusanyiko wa watu walioongozwa na Meya wa Arusha kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba kwenye ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Tukio hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Madiwani, Waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa dini (Wakristo na Waislamu) lilifanyika kwenye eneo la shule hiyo ya Lucky Vicent ambapo wakati wakiendelea kuzungumza wakiwa gorofani ghafla waliona Polisi wamefika kwa spidi na kusema watu wote wako chini ya ulinzi.
Baada ya hapo Polisi waliwakamata na kuondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari wapatao kumi ambapo baada ya kufika kituo cha kati cha Polisi, Waandishi hao waliachiwa huru huku Polisi wakiwaambia hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la tukio.

Kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika dakika chache baadae, Polisi walisema alieamuru Waandishi kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni hakufahamu kwamba hao ni Waandishi na kwamba Wanahabari hao hawana kosa lolote na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.
Kufuatia tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio hilo.
"Tulikuwa tunahangaikia wenzetu waachiwe kwanza na hatimaye tumefanikiwa,wameachiwa huru bila masharti yoyote....maelezo ya kaimu RPC yanakera na kuchekesha,na kwa kweli ni kama kejeli....Eti waandishi hawakukamatwa bali walipewa 'lift' na Polisi kuwarudisha mjini wakati walienda na magari yao na yamebaki shuleni Lucky Vincent,ni jambo gumu kueleweka",ameeleza mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Claud Gwandu.
"Awali waliambiwa kuwa wamekamatwa kwa kukutwa kwenye mkusanyiko usio na kibali lakini waliokamatwa ni waandishi 9, meya wa Arusha,diwani mmoja na viongozi wawili wa dini..Hivyo basi,uongozi wa APC,pamoja na kulaani unyanyasaji huo wa wazi kwa .maelezo ya kina kuhusu kukamwaandishi wa habari,utaandika barua ya malalamiko kwa uongozi wa Polisi Mkoa kutaka atwa kwa wanahabari hao na baada ya hapo utachukua hatua stahiki",ameongeza Gwandu.
Katika hatua nyingine meya wa jiji la Arusha,madiwani,walimu,mmiliki wa shule ya lucky Vincent,viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa masharti kwamba watakapoitajika muda wowote wafike.
Inaelezwa kuwa wamepewa dhamana baada ya polisi kutaka hizo rambirambi zikabidhiwe kituoni hapo ili ufanyike utaratibu mwingine wa kuwafikishia walengwa jambo lililopingwa vikali na meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad