MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi. Alisema mwaka wa kwanza wa serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi. Alisema serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati.

No comments:
Post a Comment