Muziki : Roma Apatikana akiwa amejeruhiwa Mkono na Mguu - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Apr 2017

Muziki : Roma Apatikana akiwa amejeruhiwa Mkono na Mguu


Msanii Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki amepatikana na sasa yupo katika kituo cha Polisi cha Oyesterbay jijini hapa.

Kaka wa Roma,Omar Musa amesema Roma alirudishwa nyumbani saa tisa alfajiri leo, na kwa sasa yupo kituo cha Oyesterbay.

Hata hivyo Omar hakutaka kueleza kwa kina kuhusu kurejea kwa Roma akisema kuwa hadi familia itakapotoa tamko.

Roma na wenzake wanne, walitekwa wakiwa katika studio za Tongwe, zilizopo Masaki, jijini hapa hivi karibuni. 


Tuendelee kusubiri watakachosema Familia na Roma Mwenyewe Jumatatu....!

Post Top Ad