Michezo : Timu ya Simba SC yatua Geita - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 4 April 2017

Michezo : Timu ya Simba SC yatua Geita


MSAFARA wa Kikosi cha timu ya Simba kimewasili salama jana jioni mkoani Geita ambapo watakaa kwa muda wa siku tatu kabla ya kueleka Jijini Mwanza kwa mechi mbili za ligi kuu Vodacom.


Simba waliotokea Mkoani Kagera walipokuw ana mechi dhidi ya Kagera Sugar waliingia mkoani Geita na kulakiwa kwa shangwe kubwa na wanachama pamoja na mashabiki wa timu hiyo na kuwataka wajihisi wapo nyumbani.


Kikosi cha wanamsimbazi kitaweka kambi ya siku tatu pia kinaweza kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Geita ya mkoani humo ikiwa ni moja ya maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu



Gari ya timu ya Simba ikiingia Mkoani Kagera wakiongozwa na msafara wa mashabiki wa timu hiyo.

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Laudit Mavugo akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.

Mwinyi Kazimoto akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita

Beki wa timu ya Simba raia wa Kongo Besela Bukungu akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.

Beki wa Simba Abdi Banda akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.


Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.


Mashabiki watimu hiyo wakiwa na shangwe za kuipokea timu yao.

No comments:

Post a Comment