Matukio : Baadhi ya Watuhumiwa Wagoma Kushuka kwenye Gari la Magereza Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Apr 2017

Matukio : Baadhi ya Watuhumiwa Wagoma Kushuka kwenye Gari la Magereza Jijini ArushaMahabusu wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha, baadhi yao wamegomea kushuka katika gari la magereza

kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao

Watuhumiwa wa ugaidi baadhi yao wakiingia katika gari la magereza baada ya 32 kutii amri ya mahakama

Watuhumiwa wa ugaidi wakiwa katika viwanja vya mahakamani jijini Arusha

Na Pamela Mollel,Arusha


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mahabusu wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha baadhi yao leo wamegomea kushuka katika gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao


Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya mahakama majira ya saa 9:27 asubuhi ambapo tukio hilo lilisimamisha shughuli za mahakama kwa muda wa zaidi ya masaa mawili huku baadhi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi wakivua nguo zao kushinikiza kesi zao kusomwa


Mahabusu 32 tu ndio waliokubali kushuka katika gari hilo na kuingia mahakamani huku 29 wakigomea kushuka na kubakia ndani ya gari hali iliyozua taharuki kwa baadhi wa watu walikuja kufatilia kesi hiyo


Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Nestory Baro aliwataka watuhumiwa hao kuwa wavumilivu, kwa kuwa kesi yao ipo katika hatua za mwisho huku akiwasii kutogomea kuja mahakamini kwa kufanya hivyo wanajinyima haki yao ya kisheria


Wakizungumza kwa nyakati tofauti mahakamani hapo watuhumiwa hao Shabani Idi na Yusuph Alli waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kwa kuwa familia zao zinaishi katika wakati mgumu


“Mtoto wangu wa darasa la nne amekatisha masomo anaokota makopo kwaajili ya kuuza ili familia wapate chakula pamoja na wadogo zake kupata nauli ya shule”alisema Shabani


Aidha waliongeza kuwa familia zao sasa zipo hatarini kuingia katika makundi mabaya ya tabia kutokana na wazazi wao kuwa mbali nao hivyo wao kuendelea kuwepo magerezani ni changamoto kubwa sana kwa familia zao

Post Top Ad