Mapishi na Chef Kile : Mchemso wa Ndizi Mzuzu na Nyama ya Ng’ombe - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Apr 2017

Mapishi na Chef Kile : Mchemso wa Ndizi Mzuzu na Nyama ya Ng’ombe
Mimi ni mpenzi sana wa kula ndizi mzuzu, ikiwa za kuchoma, kukaanga na mafuta au hata kuzichemsha. Mapenzi yangu hayo yamepelekea leo mie kuja na pishi hili zuri na nimeonelea ni vema nawe ulijue.
Chakula kwa watu 2
MAHITAJI
Nyama ya Ng’ombe robo
Ndizi mzuzu mbichi 5
Vitunguu maji 1
Kitunguu swaumu punje 3
Giligilani vijani vichache
Rosemary vijani vichache
Bay vijani vichache
Chumvi – kwa kiasi upendacho
Olive oil kijiko cha mezani kimoja
Pilipili- kama watumia
Karoti moja
Pilipili manga
JINSI YA KUPIKA
Kwanza chemsha nyama – sasa wakati wachemsha nyama weka chumvi, maji kwa kiasi, bay, rosemary, garlic na pilipili manga.
Angalia kiasi cha maji – lengo ni kupata supu ivo unaweza kuongeza maji
Ichemke hadi kuiva ndipo uweke vitunguu maji na swaumu pamoja na ndizi kisha acha ichemke na kuiva kwa dakika takribani 15, kishi weka karoti na ivisha tena kwa dakika 4 au 5.

Baada ya hapo mchemsho upo tayari kwa kuliwa na ni mlo kabimili. Ukiwa unapakua ndio mda wa kuweka vile vijani vya giligilani.

Kwa Maelezo Zaidi : Chef Kile Recipes

Post Top Ad