Maisha : Katibu Mkuu, Prof. Kitila Mkumbo Atembelea Mtambo wa Kuzalishia Maji, Ruvu Juu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Apr 2017

Maisha : Katibu Mkuu, Prof. Kitila Mkumbo Atembelea Mtambo wa Kuzalishia Maji, Ruvu Juu


Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ametembelea Tenki la Maji la terminal lilipo karibu na chuo kikuu cha ardhi ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu na chini.


Pia ametembelea tenki kubwa jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na ametembelea Ofisi za Dawasco Mkoa wa Kibaha na kumalizia ziara yake kwa kutembelea mtambo wa kuzalishia Maji wa Ruvu juu ambapo umeanza kuzalisha maji mapya.
Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa ameambatana na Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco,mhandisi, Cyprian Luhemeja katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa DAWASA, mhandisi Romanus Mwangingo, akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhusu tenki jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mtambo huo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani. 

Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco, mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakimsilikiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo

Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana.

Sehemu ya mtambo wa kusafirishia maji.









 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad