Kushoto ni msanii wa Bongo Fleva, G nako na Rayton Kwembe Mkurugenzi wa Nuru Coffee Chapchap wakizungumza na Wanahabari (Hawapo pichani)
G Nako kuzindua bidhaa bora ya Nuru Coffee Chapchap
Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam, April 2017: DMG Tanzania, kampuni tanzu ya chakula na vinywaji nchini, imezindua bidhaa yenye mchanganyiko wa kahawa, maziwa na sukari ya “Nuru coffee Chapchap” yenye hadhi ya kimataifa na ladha thabiti.
Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka kufuatia changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea nchini ikiwa na dhumuni la kulenga kila Mtanzania kuonja ladha mpya ya Nuru coffee Chap chap ikipatikana nchini kote nchini na katika masoko yote.
Kutokana na ubunifu wa DMG Tanzania unaowatofautisha na wapinzani wake katika soko, kampuni hii imewawezesha Watanzania hata ya hali ya chini, kuwa na uwezo wa kuonja ladha murua yenye mchanganyiko wa maziwa, sukari na kahawa kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh 500=/
Akizungumzia bidhaa hiyo mpya ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa Nuru Coffee Chapchap anasema “ Nuru coffee Chapchap ni bidhaa ya kipekee na ni moja kati ya bidhaa madhubuti katika kampuni yetu. Nuru ni neno la Kiswahili linamaanisha “mwangaza” ikiwa na maana ya asili, Nishati, na matumaini . Nuru huondoa giza na kuweka dhahiri vitu vilivyofichika. Nuru hung’aa popote na kurudisha tumaini kwa watu waliokata tamaa.”
Hivyo uzinduzi wa kahawa ya Nuru coffee Chapchap imekuja kwa wakati muafaka na kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa za ajira zinazotolewa nchini na kampuni hii.napia bidhaa ya nuru coffe imekuwa nuru kwa watanzania kwani imewawezesha kujipatia chai yenye mchanganyiko wa sukari maziwa na kahawa kwa gharama nafuu kabisa kwa kuzingatia hali yetu uchumi.
“Tunayofuraha kubwa kuzindua bidhaa hii ya kiwango cha juu itakayokidhi maisha ya mtumiaji, kwa kumpatia ladha nzuri ya kahawa bora kabisa na chapchap. Nuru coffee Chapchap inatokana na aina mbili kuu za kahawa nchini, Robusta na Arabika kwa asilimia 100 na kutengenezwa kwa mchanganyiko madhubuti wa maziwa na sukari, ili kuleta ladha nzuri ya kuvutia. Tumejipanga na tuna ujasiri mkubwa juu ya bidhaa yetu mpya na hivyo hatutatetereka.” Alisema ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Hivi sasa Nuru coffee Chapchap inapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Dodoma na Arusha, na pia bidhaa hii inatarajiwa kupatikana mikoa mingine nchini miezi michache baadae.
Katika kusherekea uzinduzi wa Nuru Coffee Chapchap katika soko la nchini Tanzania kampuni ya DMG Tanzania imeandaa kampeni itakayohusisha supamaketi kubwa mbalimbali kama TSN Supermarkert iliyopo kibo complex, American Super Markert pugu road na Nakumatt Mlimani City. Kampeni hiyo pia itahusisha upatikanaji wa nuru Coffee katika mitaa mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 – 25 Aprili mwaka huu.
Kitu kikubwa Zaidi katika bidhaa ya Nuru coffe ni utaalamu wa usindikaji wa bidhaaa hiyo na ufungaji wa paketi zake zinazolenga kuibua hisia ya mtumiaji kabla hata hajainunua.
Nuru coffee Chapchap wafurahia kumtaja na kumtambulisha George Sixtus Mdemu, (G Nako) ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya “maarufu kama Bongo Fleva” kuwa balozi wa bidhaa ya Nuru Coffee Chapchap nchini Tanzania. G Nako atakuwa akiitangaza bidhaa ya Nuru coffee Chapchap katika soko la Tanzania pamoja na vyombo vya habari kama radio, TV, magazeti na mitandao ya kijamii.
Pamoja na mambo mengine G Nako kama balozi wa Nuru coffee Chapchap atakuwa akishirikiana pamoja na wateja wetu kueneza bidhaa yetu yenye ubora wa hali ya juu.
“Tunayo furaha kubwa na tunategemea G Nako ataeneza uwezo wa bidhaa yetu na kuwa balozi madhubuti. Tunajivunia kazi tunayoendelea kufanya pamoja naye na tunategemea kuimarisha uhusiano wetu kwa kuikuza lebo yetu na kuieneza kote nchini” Alisema Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
“Mimi pamoja na Nuru coffee Chapchap tumekuwa na uhusiano thabiti, DMG Tanzania ni kampuni nzuri na ninajivunia kufanya kazi pamoja nayo, “ G Nako.
DMG Tanzania haitabaki nyuma katika kuhakikisha inaongeza ubora katika bidhaa yake ya Nuru coffee Chapchap na pia inampango wa kuzindua bidhaa nyingine nyingi chini ya mwamvuli wa lebo ya Nuru. Ikiwa na lengo la kukuza usambazaji wa bidhaa yake DMG Tanzania inalenga kuifikia Tanzania yote pamoja na Africa Mashariki.
KUHUSU DMG
DMG Tanzania inadhamira ya kubadili hali ya sasa ya Tanzania ikiwa ni kukuza ushirikiano wa kibiashara. Tuna lengo dhabiti la kujifunza kutoka nchi nyingine kama Korea ili kupata uzoefu wa kiteknolojia na kupata ujuzi ili kujenga undugu na ushirikiano hapa Tanzania.
Tumedhamiria kusambaza kahawa nzuri na yenye kiwango kizuri cha kahawa, maziwa na sukari ili kuleta ladha mpya kwa watumiaji.
Nuru coffee Chapchap ina gramu 120 (12g × 10pks) ikiwa na mchanganyiko kama ifuatavyo:- kahawa 5.5%, sukari, Nondairy cream [glucose syrup, hydrogenated oil palm, sweet whey powder, sodium caseinate, potassium phosphate], dextrin, silicon dioxide, nature identical hazelnut flavor
Kwa sasa Nuru coffee Chapchap inazalishwa nchini Korea ya Kaskazini ingawa tunategemea kwa siku za karibuni iwe inazalishwa hapa nchini.
DMG Tanzania inadhamira ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha masoko yote na baadae kuenea sehemu nchi zote za jirani ikiwa ni pamoja na ukanda wa mashariki kati na kusini mwa Afrika. Pia DMG Tanzania inalenga kuitangaza Nuru coffee chapchap ili kufikia lebo kubwa zaidi nchini Tanzania.
Kwa maelezo zaidi tembelea
Facebook;https://www.facebook.com/Nuru-Coffee-Chapchap
Instagram; @nurucoffeechapchap
No comments:
Post a Comment