Habari : Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe azindua vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya Sh.Milioni 100 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Apr 2017

Habari : Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe azindua vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya Sh.Milioni 100



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) Dkt. Herbet Makoye pamoja na viongozi wengine na watendaji wa TaSUBA wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye pamoja na watendaji mbalimbali wa Wizara na wa taasisi hiyo kuelekea kuangalia maeneo mbalimbali ya taasisi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi maji ya bahari yalivyoharibu kingo za taasisi hiyo wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akionyeshwa baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya Studio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipiga nyimbo kwa kutumia kinanda ndani ya moja ya Studio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.






Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizindua rasmi vifaa vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi za picha za kuchora toka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA) pamoja na watendaji wengine wa Wizara mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA), Watendaji waWizara pamoja na wageni toka nje ya nchi mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)




Na Lorietha Laurence.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilling 100 kwa ajili ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) vitavyowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo namna ya kutengeneza picha jongefu.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Wilayani Bagamoyo, Dkt.Mwakyembe amesema kuwa vifaa hivyo ni muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wa Taasisi hiyo katika kuwaongezea ujuzi katika vitendo na baadaye kuwa watendaji bora na makini.


“Vifaa hivi ni tija katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa vitendo na hivyo kuzalisha watu wenye taaluma zenye tija na zenya kuleta matokeo chanya kwa ajili ya maendeleo nchi”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.


Aliongeza kwa kuhaidi kuwa atahakikisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Mabalozi wanapata fursa ya kuitembelea TaSUBa ili wajionee kwa macho hazina kubwa waliyonayo katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni.


Aidha aliupongeza viongozi na walimu wa TaSUBa kwa jitihada wanazozifanya za kutoa elimu kwa vijana jambo ambalo linawajengea uwezo wa kujiajiri kupitia taaluma ya sanaa hivyo kuondoa utegemezi na kukuza uchumi wa nchi.


Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bibi Erica Yegela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) ipo kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote na hivyo wanakaribishwa kujiunga na kujifunza sanaa,utamaduni na uandaaji wa vipindi.


Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za maendeleo kiasi cha shilling millioni 100 amabazo zimefanikisha kununua vifaa vya kufundishia kwa vitendo.


“Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia kiasi hiki cha fedha ambapo kwa kiasi kikubwa kimefanikisha manunuzi ya vifaa hivi vya kufundishia na huu ni mwanzo mzuri nasi tunaahidi kutumia ipasavyo katika kuzalisha wanataaluma hodari” alisema Dkt. Makoye.


Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kufanikiwa katika kununua vifaa kumekuwapo na changamoto mbalimbali zinazoikabili- Taasisi hiyo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi huku wengi wao wakiwa wamestaafu,uhaba wa ofisi za waalimu na wafanyakazi pamoja na miundo mbinu chakavu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad