Tuzo : Mohammed Dewji ashinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bora Afrika 2017 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Mar 2017

Tuzo : Mohammed Dewji ashinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bora Afrika 2017


Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa mwaka 2017 inayotolewa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Afrika (Africa CEO Forum). Dewji ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda Abdulsamad Rabiu (CEO wa BUA Group), Issad Rebrab (CEO wa Cevital), Naguib Sawiris ( CEO wa OTMT Investments), Said Salim Awadh Bakhresa (CEO wa Bakhresa Group) na Strive Masiyiwa (CEO wa Econet). Akizungumza kuhusu ushindi huo, Dewji ameishukuru Africa CEO Forum kwa kutambua mchango wake kwa kumchagua kuwa mshindi tuzo hiyo lakini pia kuwashukuru Watanzania na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya kudhibiti na kubana matumizi mabaya ya pesa ya umma. “Ninashukuru sana Africa CEO Forum kwa heshima hii ambayo mmenipa, napenda kutoa tuzo hii kwa nchi yangu Tanzania, bila wao nisingekuwa hapa na MeTL Group isingekuwa katika nafasi iliyonayo sasa, nawashukuru sana kwa kuniruhusu mimi na familia nzima ya MeTL kukua na kufika hapa, “Pia napenda kutoa heshima kwa Rais wangu John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri na wote tunajua Afrika inavyokabiliwa na vitendo vya rushwa lakini yeye ni mmoja wa watu ambao wanapambana na rushwa, kubana matumizi mabaya na wenye mwono katika kazi yake.” alisema Dewji. 


Aidha Dewji alisema kwa sasa bara la Afrika uchumi wake unakua kwa kasi huku akitolea mfano wa ripoti yam waka 2015 ambayo ilionyesha uchumi wa Afrika unakua kwa asilima 4 kwa mwaka kulinganisha na Ulaya inayokua kwa asilimia 1.5 hivyo kuwashauri wanachama wa Afrika CEO Forum kutumia vyema fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi. Washindi wengine wa tuzo zilizotolewa na Africa CEO Forum ni; CEO of the Year
Abdulsamad Rabiu, CEO, BUA Group
Issad Rebrab, Chairman, Cevital
Mohammed Dewji, CEO, MeTL - WINNER
Naguib Sawiris, Chairman, OTMT Investments
Said Salim Awadh Bakhresa, CEO, Bakhresa Group
Strive Masiyiwa, CEO, Econet

Young CEO of the Year
Anta Babacar Ngom Bathily, DG, Sedima - WINNER
Basil El-Baz, PDG, Carbon Holdings
Darshan Chandaria, PDG, Chandaria Industries
James Mworia, PDG, Centum Investments
Mohamed Ben Ouda, DG, SNTL
Lamia Tazi, DG, Sothema

African Company of the Year
CIEL Group
ECONET
Elsewedy Electric - WINNER
Label’Vie
MTN
OCP Group

African Bank of the Year
Attijariwafa Bank - WINNER
Banque Centrale Populaire
Ecobank
Mauritius Commercial Bank
Standard Bank Group
. United Bank For Africa

Private Equity Investor of the Year
Actis
Afrinvest - WINNER
Development Partners International LLP
Helios Investment Partners
Leapfrog Investments
The Abraaj Group

International Corporation of the Year
Allianz - WINNER
Coca-Cola
Mota-Engil
Orange
Siemens
Vitol

Tuzo za Africa CEO Forum zimetolewa Geneva, Switzerland ambapo wanachama wa jukwaa hilo wapo katika mkutano wa siku mbili wakijadili mambo mbalimbali ambayo yanawahusu wao kama Watendaji Wakuu na jinsi gani wanaweza kulisaidia bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad