Matukio : DC Dodoma akutana na Kamati ndogo ndogo ya Mkoa ya Uratibu Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Mar 2017

Matukio : DC Dodoma akutana na Kamati ndogo ndogo ya Mkoa ya Uratibu Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa KimataifaMkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na Kamati ndogo ya Mkoa inayoratibu Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utakojengwa katika kata ya Nala Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.

Mjumbe wa hiyo ambaye ni Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) wakati Kamati hiyo ilipokutana na Mkuu huyo wa Wilaya.

Mjumbe wa hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Dodoma Bw. Hashimu Kitambuliyo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) kuhusu mipango na mikakati iliyoweka na Kamati hiyo katika kufanikisha Mradi huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

Post Top Ad