Siasa : Madiwani waoga Nitawakana mbele ya Wananchi - Lema - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Mar 2017

Siasa : Madiwani waoga Nitawakana mbele ya Wananchi - LemaMbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha.

Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,wa kwanza kulia ni Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma

Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha Jana.

Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo jana jijini Arusha.

Na,Vero Ignatus ,Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoika rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.


Ameyataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .

Post Top Ad