Maisha : JK, Mzee Mwinyi Wahudhuria Mazishi ya Sir George Kahama Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Mar 2017

Maisha : JK, Mzee Mwinyi Wahudhuria Mazishi ya Sir George Kahama Jijini Dar es Salaam



Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Mjane wa Marehemu Sir George Kahma, Mama Janeth Kahama akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akiweka udongo katika kaburi

Marais Wastaafu na wake zao pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.




Sehemu ya ndugu wa familia Marehemu Sir George Kahama wakiwa mazishini katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam

Sehemu ya ndugu wa familia Marehemu Sir George Kahama wakiwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam

Sehemu ya ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya Marehemu Sir George Kahama wakiwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi na wake zake Mama Sitti Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Sir Georeg Kahama

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua kaburini

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe mama Evelyne Warioba wakiweka shada la maua kaburini

Mawaziri Nape Nnaue ya Mwigulu Nchemba wakiweka shada la maua kaburini

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua katika kaburi

Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman akiweka shada ya maua kaburini

Waziri wa Mambo ya Nje Mstafu Mhe. Bernad Membe akiweka shada la maua kaburini

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Mstaafu Rashid Othman akiweka shada la maua kaburini

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiweka shada la maua kaburini



Mhe. Andrew Chenge na mkewe wakiweka shada la maua kaburini

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga akiweka shada la maua kaburini

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa mazishini katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuele Massaka wa Globu ya Jamii.



KABLA YA MAZISHI...


Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa salamu za pole katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Makamu wa Rais mstaafu katika Serikali ya awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Mjane wa Marehemu Sir. George Clement Kahama Mama Janet Kahamawa (pili kushoto) akiwa na familia yake wakati wa Tukio la kumuaga mume wake ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu za pole kutoka Serikalini katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdurahaman Kinana akitoa salamu za rambirambi za Chama wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Jaji Mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.


Serikali imesema itaendelea kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania maendeleo na ustawi wa jamii uliofanywa na marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.


Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa Taifa na Waziri msataafu marehemu Sir Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Waziri Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na aliyetekeleza majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa viongozi walioanzisha harakati za Serikali za uendelezaji wa mji wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha makao makuu ya nchi.


“Marehemu Sir George Kahama tutamuenzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya katika kuijenga nchi yetu hasa katika ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa nchi”.Alisema Waziri Nape.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdurahaman Kinana amumueleza Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa hali ya juu na alikuwa mchapakazi.


“Sir George Kahama alikuwa mtumishi na kiongozi aliyetukuka ametuachia hamasa kubwa ya kuwa viongozi bora zaidi na wenye mapenzi na Taifa letu katika kuleta maendeleo.”Alisema Ndugu Kinana.


Marehemu Sir George Kahama amekuwa Waziri na Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa leo Jijini Dar es Salaam na ameacha Mjane na Watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad