Utalii/Filamu : Kampuni Maarufu ya Filamu ya Ujerumani kupaisha sekta ya Utalii nchini - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Dec 2016

Utalii/Filamu : Kampuni Maarufu ya Filamu ya Ujerumani kupaisha sekta ya Utalii nchini


Moja ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara na inatarajiwa kukuza utalii . 
Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha(kushoto)Gabriel na Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouder wakiwa eneo la kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi. 
Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouderk(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati) anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha,Gabriel.
Mratibu wa Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Mona Lessink akizungumza na waandishi wa habari kuhusu filamu hiyo itayoanza kurushwa katika kipindi cha Pasaka mwaka 2017,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal shulutete akifatilia kwa karibu.
Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni 
Wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa eneo la kutengeneza filamu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti 


Askari wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa Serengeti wakiimarisha ulinzi kwa wageni hao 
Katika kuboresha filamu hiyo upigaji wa picha kwa kutumia ndege ndogo ili kuonyesha madhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ulifanyika chini ya usimamizi wa Tanapa.
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (katikati) akizungumza na Mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon ya nchini Ujerumani,Mona Lessnick alipotembelea eneo la Kogatende jirani na  Mto Mara ambapo kulikuwa kukifanyika shughuli za uchukuaji wa picha za video kwa ajili ya Tamthiliya ya Dream Boat.kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mratibu wa uzalishaji wa Filamu wa kampui ya Polyphon Studio,Mona Lessnick (kulia) akiwa na Mpiga picha mkuu wa kampuni hiyo ,Manuel Schroeder na Jorg Gariel  wakati wakizungumza na wanahabari  (hawapo pichani) juu ya tukio la uchukuaji wa picha za video katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo picha za video za sehemu ya Tamthiliya ya Dream Boat zimepigwa hapo.
Moja ya gari lililotumika katika tukio hilo likitoka eneoo la tukio kando ya Mto Mara unopita katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Uchukuaji wa picha za video kando ya Mto Mara ukiendelea.
Magari yakiwa yamebeba sehemu ya vifaa kwa ajili ya uchukuaji wa picha za Video.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiteta jambo na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa( katikati) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Jorg Gabriel walipoktana eneo la Kogatende katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akisaidia kubeba moja ya Kamera kubwa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uchukuaji wa picha katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Moja ya Kamera kubwa iliyokuwa ikichukua matukio katika upigaji picha wa Tamthiliya ya Dream Boat katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii akiitizama Kamera ambayo ilikuwa iktumika kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo.
Wataamu wakifunga Kamera katika ndge ndogo ya Shirika la ndege la Costal Airline kwa ajili ya upigaji wa picha za juu . 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

SEKTA ya Utalii nchini inatarajia kupiga hatua baada ya wasanii maarufu wa filamu kutoka nchi za nje kuanza kutumia baadhi ya maeneo katika vivutio vya Utalii vilivyoko nchini kuandaa sehemu za tamthiliyaa zao.

Kampuni kubwa ya utengezaji wa filamu ya Polyphon Group  ya Humburg  nchini Ujerumani imekuwa ya kwanza kupiga picha za video za sehemu ya tamthiliya maarufu nchini Ujerumani ya Dream Boat ambayo imekuwa ikiooneshwa katika vituo mbali mbali vya televisheni kwa nchi zinazozugumza lugha ya Kijerumani.

Maeneo ambayo picha za video zimechukuliwa ni pamoja na Kogatende na Lobo ndani ya Hifadhi za Taifa za Serengeti ,huku picha nyingine zikipigwa katika Hifadhi ya taifa ya Arusha pamoja na Pori la akiba Endumeti.

“Tumefanya Sehemu moja ya Tamthiliya yetu Botswana,moja Zambia na nyingine Kenya katika muendelezo wa tamthiliya hii inayooneshwa kwa mika 30 sasa,Sehemu ya mwisho ya muendelezo wa filamu hii iliyochukuliwa Afrika ilikua mwa 2007,ni muda mrefu na tuliangalia wapi tunaweza enda,na tukafanya utafiti ,tukaja Tanzania,Tumeona hii nchi ni nzuri tukaamua kuleta filamu yetu hapa”.alisema Manuel Schroeder mpiga picha wa kampuni ya Polyphon Studio.

Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa amesema hatua hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii kimataifa huku mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon,Mona Lessnick akieleza utalii utaongezeka kupitia tamthiliya hiyo.

“Kutokana na uzoefu ,watu wametuamini sisi , tumefanya hii kazi kwa miaka 30 sasa,hivyo baada ya kurusha sehemu ya tamthiliya ilichukuliwa hapa itaongeza soko la wageni kutoka nchi zinazozungumza kijerumani,kwa sababu wanajua tunafanya utafiti,tmekwisha fka hapa mara mbili na kukutana na mtaalamu na kutuonesha maeneo ,wanajua tunachukua maeneo mazuri,hoteli nzuri,tuna taarifa  na vifaa vya kutosha,hivyo kutakuwa na matokeo makubwa katika Utalii “alisema Lessnick.

Kuhusu Maudhui ya Tamthiliya hiyo ambayo inaoneshwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa ,Mona Lessnick amesema imebeba maudhui ya aina tatu ambayo ni Vichekesho,Mahusiano pamoja na Drama.
“Ni Burudani kwa familia,tuna hadithi tatu,katika hadithi kuu watu wanasafiri kwa meli kuizunguka nchi,wakasafiri kuja Tanzania ,kuna hadithi nzuri za mahusiano ambazo vipande vyake vimechukuliwa Tanzania “alisema Lssnick.

“Katika muongozo tuna aina tatu ya hadithi,tuna hadithi ya mapenzi,tuna hadithi ya vichekesho na drama hii tunayofanya leo ni vichekesho,tuna watu wawili ,katika muongozo wa kwanza inaonesha watu haw wamepata tatizo katika gari lao hapa  Serengeti,lakini tulipaa ugumu kupiga picha ndio tukapata mahala hapa pazuri kwa kufanya video,tukafanya Drama hapa ya gari kukwama ndani ya maji na gari nyingine ikaja nyuma kuoka watu hawa wakiw wamekaa juu ya gari lao na kuondolewa katika maji”alisema Schroeder.

Tamthiliya ya Dream Boat imefikisha miaka 35 sasa tangu kuanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya Televisheni nchini Ujerumani na kwamba sehemu mbili zenye urefu wa dakika 90 kila moja za tamthiliya hiyo ,picha zake hupigwa katika nchi moja ya kiafrika .

Post Top Ad