Utalii Wetu : JWTZ na Wanahabari katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Dec 2016

Utalii Wetu : JWTZ na Wanahabari katika Kilele cha Mlima KilimanjaroSafari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.

Safari ilikuwa ni usiku kuchaJua likachomoka wakati safari ikiendelea.Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.

Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.

Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba.

Safari ya kuelekea Uhuru Peak ikiendelea.

Hatimaye wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga.


a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati.


Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini aliyekuwepo katika safari hiyo.

Post Top Ad