Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wakati wa kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero, ambapo alimshukuru kwa jitihada zake katika kusaidia upatokanaji wa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Barabara, nishati, kilimo na elimu, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero wakifurahia uhusiano mzuri uliopo kati ya Benki ya AfDB na Tanzania ambapo mpaka sasa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo inafikia thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2, wakati wa kuagwa kwa Dkt. Kandiero, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero akitoa maneno ya shukrani mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati akiagwa na Waziri huyo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), baada ya kuagwa rasmi, katika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia) wakati akiagwa rasmi baada ya kupewa majukumu mengine ya Ukurugenzi Mkuu wa Benki ya AfDB kusini mwa Afrika, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa tayari kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero baada ya kufanya kazi nchini kwa takribani miaka sita, Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).