Teknolojia : Airtel Fursa yazidi Kunufaisha Vijana mikoa ya Lindi na Mtwara - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Dec 2016

Teknolojia : Airtel Fursa yazidi Kunufaisha Vijana mikoa ya Lindi na Mtwara


Vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara walioendelezwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wa Airtel Fursa wamesema tayari wameanza kupata mafanikio kutokana na Ongezeko la Faida za kiuchumi ambazo zinatokana na kuwezeshwa na kampuni hiyo.
Hali hiyo imeonekana baada ya Kampuni ya Airtel Kuwatembelea katika maeneo wanayofanyia Biashara mara baada ya kuwawezesha na kusimamiwa na Viongozi wa Airtel wa mkoani kwa lengo la kutazama changamoto pamoja na mafanikio wanayoyapata.
Mkoani Mtwara mmoja wa mnufanika anaonekana kuboresha eneo lake la biashara baada ya kufungua ofisi nyingine ili kujipatia faida maradufu huku kikundi cha Sauti ya Jamii kilichopo Lindi kinachojishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji kilipokea msaada wa mbuzi 40 kuonekana kupata changamoyo na kuanza upya.
“Tunaishukuru sana Airtel kwa msaada wa mbuzi 40 pamoja na kutujengea banda la kisasa hapo mwanzo, tumeeendea vyema lakini tukapatwa na changamoto ya baadhi ya mbuzi wetu kupatwa na ugonjwa na kufa, tulijipanga upya kwasasa tuliuza wale wote kama nyama na sasa tumenunua mbuzi wazuri wanaweza kuzaa mapcha kila mzao, sasa tunaamini tutanza kuona faida alisema” Salum Muunguja-Katibu kundi la Sauti ya Jamii.

kwa upande wa mjasiliamali wa Airtel Fursa Mtwara Bi. Prisca Chilumba ambae anafanya ujasiliamali wa Saloon saloon ya kike alisema “Mimi kwa kweli naishukuru sana Airtel Fursa kwa kuniwezesha binafsi nimeweza kujipatia kipato cha kunitosha na hadi sasa nimeweza kuboresha ofisi yangu na kuhamia sehemu kubwa zaidi, pia ninamuda hata kujitangaza na kujitolea kwa wengine kwa lengo la kupanua masoko mkoani hapa”.



Naye meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando anasema changamoto katika ujasiliamali ni hali ya kawaida hivyo vijana waliowengi wanapaswa kujifunza zaidi ili kuweza kujikwamua katika dimbwi la umasikini.
Changamoto kwa mjasiliamali ni kitu cha kawaida sana, sisi Airtel tunafanya ziara za kuzunguka na kufahamu maendelea au changamoto za vijana wote waliosaidiwa na Airtel FURSA ili kujua ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia waendelee kufikia ndoto zao, tayari tumeshapita tumeshaandaa mkakati wa kuwasaidia wote hivyo tunachotaka ni jamii pia kuwaunga mkono vijana hawa ili waweze kufikia malengo waliojiwekea na hatimae kusaidia jamii pia” alieleza Mmbando

Post Top Ad