Matukio : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa azindua mradi wa Umwagiliaji Karatu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Dec 2016

Matukio : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa azindua mradi wa Umwagiliaji Karatu




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision,,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Miradi katika shirika hilo Revocatus Kamara.Picha na Ferdinand Shayo


Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.



Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua mradi wa Umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karatu uliofadhiliwa na Shirika la Worlvision ambao unahudumia ekari 1200 na kuwafikia wakulima 4000.


Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo ,Majaliwa amesema kuwa mradi huo utasaida kuchochea kilimo cha umwagiliaji hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya tabia ya nchio na uhaba wa mvua.


Majaliwa amesema kuwa Asilimia 80% ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo idadi ambayo ni kubwa hivyo kilimo cha umwagiliaji kikihamasishwa ipasavyo wakulima watapata tija kubwa na kuinua pato la taifa.


Aidha amelishukuru shirika la Word vision kwa kujitoa kusaidia jamii katika eneo hilo muhimu la kilimo ambalo ni tegemeo kwa wakulima wengi.


Waziri Mkuu ameonya tabia ya baadhi ya watu wanaohujumu vyanzo vya maji kwa kuunganisha mashine katika vyanzo na kufanya uharibifu hivyo amewataka kuondoka mara moja katika chanzo hicho na iwapo watakaidi serikali itawachukulia hatua kali.


Mkurugenzi wa Miradi katika shirika la World Vision Revocatus Kamara amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wakulima wengi na kupelekea upatikanaji wa chakula pamoja na kukuza kipato cha wakulima.


Kamara amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana vyema na serikali ili kufanya miradi itakayosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Post Top Ad