Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Kibuyuni Kata Panzuo, alipokuwa katika ziara yake ya kuwashukuru
wananchi kwa kumchagua, pia kusikiliza kero zao, hususani ile ya Mifugo
kuharibu vyanzo vya maji pamoja na mazao yao.
Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Mkuruwili, alipokuwa katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwa
kumchagua, pia kusikiliza kero zao.
Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na
wachezaji wa timu ya Mbulali FC inayo shiriki kombe la Ulega.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Nyatanga FC.
IGA yatoa mafunzo ya Usimamizi wa Miradi ya Jotoardhi
Na Johary Kachwamba - TGDC
Wataalamu kutoka Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (International Geothermal
Association-IGA) wametoa mafunzo ya usimamizi wa miradi ya jotoardhi kwa
wataalamu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC).
Mafunzo haya yanafadhiliwa na Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya
Benki ya Dunia (ESMAP) katika jitihada za kuijengea uwezo TGDC ili iweze kusimamia
miradi ya jotoardhi ambayo bado ni teknolojia ngeni nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Meneja Mkuu TGDC,
Mhandisi Kato Kabaka alitoa shukrani kwa ESMAP na kusema “ni fursa muhimu kwetu
kama kampuni katika maandalizi ya kuendeleza nishati ya jotoardhi inayolenga kusaidia
taifa kufikia malengo yaliyo katika dira ya 2025”.
Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki
ya Dunia (ESMAP) Dkt. Thrainn Fridrikson aliwapongeza TGDC kwa jitihada walizofikia
na kuahidi kuendeleza ushirikiano na TGDC pamoja na IGA wakati wote wa mchakato
wa kuwajengea uwezo wataalamu wa jotoardhi nchini.
Mhandisi Uchorongaji, Amani Christopher kutoka TGDC alishukuru wakufunzi na
wafadhili kwa niaba ya TGDC “mafunzo haya yana tija sana kwetu hasa waandisi
tuliotoka katika mufunzo ya vitendo nchini Kenya kwa kuwa sasa tunaweza kuowanisha
utekelezaji na usimamizi wa miradi ya jotoardhi, hasa kipengele cha uchorongaji”
alisema Amani.
Mafuzo hayo yalihusu usimamizi katika manunuzi, taratibu za kisheria, uchorongaji na
fedha za kugharamia miradi.
Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania
(TGDC), Mhandisi Kato Kabaka akizungumza na wataalamu wa nishati ya jotoardhi
kutoka TGDC, Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia
(ESMAP) na Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo
maalum ya kuwajengea uwezo wataalamu wa jotoardhi nchini.
Mtaalamu
kutoka Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) Mhandisi Cristian
Scanzoni akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa uchorongaji visima vya
jotoardhi wakati wa miradi. Mafunzo hayo maalum yalifadhiliwa na ESMAP
na yalilenga kuwajengea uwezo wataalamu wa Jotoardhi Tanzania.
Wataalamu
wa nishati ya jotoardhi kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi
Tanzania (TGDC), Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya
Benki ya Dunia (ESMAP) na Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) katika
majadiliano wakati wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo yaliyafanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Benki ya Dunia Tanzania.
Mtaalamu
wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya
Benki ya Dunia (ESMAP) Dkt. Thrainn Fridrikson akifungua mafunzo ya
kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati ya jotoardhi nchini, mafunzo hayo
yamedhaminiwa na ESMAP na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Banki
ya Dunia Tanzania.