Arusha : Mahakama yawapa siku 10 Mawakili wa Lema - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Dec 2016

Arusha : Mahakama yawapa siku 10 Mawakili wa Lema



Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya mahakama kumalizika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo amewapa siku kumi(10)mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema .


Agizo hilo limekuja kutokana na mahamama kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa mbunge hu


Jaji Dkt.Modesta Opiyo mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa lazima.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia leo,hadi hapo Desemba 30, 2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.


****TUJIKUMBUSHE****


Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.


Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.

Post Top Ad