Bodi
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imezinduliwa rasmi na
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles John Tizeba katika
ukumbi wa Kilimo I hivi karibuni lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa
wakulima wanapata mbolea kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Mhe Dkt. Tizeba amewataka kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu ili kuweza kufika lengo kuu la kuanzishwa kwa mamlaka hii.
Amewataka wajumbe wa Bodi wawe wawajibikaji na wabunifu katika utendaji wa kazi zao.
Aidha
Jambo kubwa ambalo alilowataka wajumbe hao kuanza nalo kulifanyia kazi
ni bei ya mbolea hapa nchini ambayo ni kubwa na hivyo kupelekea wakulima
wengi kushindwa kumudu kununua.
“
Suala la kushusha bei ya mbolea liwe suala la kwanza kulifanyia kazi
kwa mstabali wa maendeleo ya kilimo chetu kwa wakulima wetu”
alifafanunua Dkt. Tizeba.
Kushusha
bei ya mbolea kutasaidia sana na kuchangia kupunguza gharama za
uzalishaji wa mazao mbali mbali kwa wadau wetu, alifahamisha Mhe. Dkt.
Tizeba.
Aliwataka
kutazama upya sheria iliyoanzisha mamlaka hii kuona kama kuna uwezekano
wa kukukabiliana na bei za mbolea ambazo zinatengenezwa kijanja kijanja
mitaani ili kumuumiza mkulima mdogo.
“
Sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Mbolea Tanzania ina upungufu kidogo
hivyo nawaomba muitazame upya ili tuweze kufanya marekebisho madogo
katika sheria hii” aliongeza Dkt. Tizeba.
Pia
Dkt. Tizeba aliwatahadharisha wajumbe kuwa wanafanyakazi miongoni mwa
watu matajiri na wanyonge sana, hivyo wajihadhari kuingia katika mtego
wa vivutio vya rushwa.
“Wajumbe
acheni tabia ya kutaka “kuonwa” na matajiri kwani mnaweza kupoteza
uadilifu katika utekelezaji kazi zenu na kujikuta mnajiingiza katika
kashfa za kukosa uaminifu” alisisitiza Dkt. Tizeba.
Mhe. Charlse Tizeba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Mshindo Msolla wa pili kutoka kushoto.
Kutokana
na hali hiyo alienda mbali zaidi kwa kuwapa pole Wajumbe wa Bodi kwa
kuwa watafanyakazi katika mazingira magumu kwani wako midomoni mwa watu
wenye fedha.
Alisisitiza
kuwa maendeleo ya kilimo hapa nchini yako mikononi mwao kwa kiasi
kikubwa kwani wao ndio chanzo cha maendeleo ya kilimo kwa wakulima wetu
waliowengi.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Mshindo Msolla amemhakikishia Mhe. Dkt.
Tizeba kuwa watafanyakazi kwa uwezo wao wote ili kufikia lengo lao.
“
Hatuwezi kukuangusha hata kidogo tutafanya kazi kwa bidii na uzalendo
wa hali ya juu kwa manufaa ya Taifa letu “ aliahidi Dkt. Msolla.
Wajumbe
wa Bodi hiyo ni pamoja na Dkt. Mshindo Msolla ambaye atakuwa ni
Mwenyekiti na anatoka Taasisi inayojishughulisha na Biashara ya Mbolea (
AFAP), Dkt. Ernest Marwa kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Dkt.
Matilda Kulumuna kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Mlingano cha mkoani
Tanga na Dkt. Mwijarubi Nyaruba ambaye anatokea Tume ya Mionzi Tanzania
( Tanzania Atomic Energy Commission).
Wajumbe
wengine ni Bw. Frank Mushi ambaye anatokea Umoja wa Wauzaji wa Mbolea
Tanzania ( TANADA), Bw. Arnold Kisinga mjumbe kutoka NEMC na kutoka
Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ni Bw. Nickonia Mwambene, Hawa Kihwele
kutoka MVIWATA na kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ni Bw. Canuth
Komba na Bw. Sospeter Mtemi.
No comments:
Post a Comment