Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati) akisaini kitabu
cha wageni alipotembelea daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni
jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kuangalia na kutatua
changamoto za wananchi ikiwa ni mwisho wa ziara siku ya pili kwenye
Wilaya hiyo (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara,
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda kuhusiana na tozo ya magari kuvuka katika
daraja la Nyerere wilayani.
Mgandilwa, amelitaka Shirika la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuangalia upya tozo ya magari kuvuka katika
daraja la Nyerere wilayani humo ikiwa ni pamija na kutaka magari yote
ya serikali na watumishi wa umma wanaofanya kazi katika halmshauri hiyo
kutokulipa tozo hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa kilio
hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul akonda, wakati wa
ziara ya mkuu huyo wa mkoa ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi
mkoani humo.
Mgandilwa alisema, kitendo cha
magari ya halmshauri hiyo na watumishi wa umma wanaoishi nje ya
halmshauri kutozwa fedha kuvuka katika daraja hilo kinaleta changamoto
kubwa na kukwamisha ufanisi.
Alimuomba Makonda kuingilia kati suala la gharama hizo na kuitaka NSSF kuziondoa kwa magari yote ya halmshauri na watumishi.
“Kila gari ya halmashari
inayopita katika daraja hili inatozwa fedha. Hasa ikizingatiwa kuwa
halmashauri hii ni mpya hivyo watumishi wengi wanatokea nje ya
halmashauri,”alisema Mgandilwa.
Alielezea changamoto nyingine kuwa
ni kipande cha Kilometa 1.5 cha barabara ya vumbi kutoka katika
daraja hilo upande wa Kigamboni.
“Hii barabara licha ya kutumiwa na
magari mengi yanayopita katika daraja hili, lakini haijajengwa kwa
kiwango cha lami hivyo wananchi kupata kero kubwa kutokana na vumbi
,”alisema Mgandilwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara akitoa ufafanuzi kuhusu suala la
tozo la daraja daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar
es Salaam.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la
tozo ya daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara,
alikiri kupokea malalamiko ya watu wengi kutaka kupunguziwa au
kuondolewa tozo hiyo.
“Ni kweli tumekuwa tukipokea
malalamiko hayo kutoka kwa wananchi mbalimbali, lakini suala ni kwamba
sisi kama NSSF huwa hatupangi viwango vya tozo za kuvuka daraja bali
tunapokea maelekezo kutoka wizara husika (Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi),”alisema Profesa Kahyaraa.
Alisema atawasilisha suala hilo katika wizara husika ili kuona uwezekano wa kuondoa tozo hiyo ama kupunguza.
Mbali na hayo, Profesa Kahyarara,
alitaja changamoto zingine kuwa ni vijana kuligeuza daraja hiyo kuwa
kijiwe na wengine kuwa na nia ovu ya kulihujumu kwa kuharibu
miundombinu, ingawa ulinzi umeendelea kuimarishwa.
Kwa upande wa Makonda, alisema,
suala la tozo ya magari ya halmashauri na watumishi kuvuka katika
daraja hilo atazungumza na waziri mwenyedhamana.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakielekea kugagua miundombinu ya
daraja hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiangalia mti
uliopandwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na
usalama pamoja na viongozi wengine wakiangali mtaro wa wakupitishia
maji katika daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na
usalama pamoja na viongozi wengine wakikagua miundombinu ya daraja hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akizungumza na wananchi
wanaoshi eneo la daraja Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar
es Salaam ilipoishia barabara ya kiwango cha lami aliposimama na msafara
wake ili kusikiliza kero na changamoto wanazozipata katika eneo hilo.
Akihutubia wananchi wanaoishi
jirani na daraja hilo,Makonda alisema, tayari mkandarasi wa ujenzi wa
kipande cha barabara cha kilometa 1.5 inayounganisha daraja la Nyerere
atanza kujenga kipande hicho kwa kiwango cha lami.
“Mkandarasi aliyejenga daraja
hili ndiyo ataendelea na ujenzi wa kipande hiki kilichobakia.Pesa zipo
na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa ujenzi utaanza,”alisema.
Wananchi
wanaoishi karibu na mradi wa daraja hilo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda (hayupo pichani) alipo simama na
msafara wake.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wananchi
aliposimama na msafara wake eneo la Kibada Wilaya ya Kigamboni jijini
Dar es Salaam.
Mkazi wa Kibada, Bi Siwazuri Abdalah akimuelezea Makonda kero anazozipata katika Hospital ya kibada.
Mkuu
wa Idara ya Uifadhi wa Mazingira na Usimamizi wa Taka Ngumu, Fanuel
Kibera akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
(katikati), mchoro wa dampo la kisasa litakalojengwa eneo la Kisarawe
II Kigamboni.
Muonekano wa eneo litakalojengwa dampo la kisasa Kisarawe II Kigamboni.
Vikosi
vya ulinzi na usalama wakisaidia kulisukuma gari la Clouds Media
liliponasa katika mchanga ene la Kisarawe II wakati wa ziara ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kukagua eneo litakalojengwa dampo la
taka la kisasa.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ukiwa eneo la Kisarawe II.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi
wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi (mwenye kanzu),
alipotembele kukagua shughuli za kiwanda hicho wakati wa ziara yake.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati), akiwa amefuatana
na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na Mkurugenzi wa
Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi (mwenye kanzu) wakiwa
ndani ya kiwanda hicho wakikagua shughuli za kiwanda hicho.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Maziwa na Maji (MILKCOM), Yusuph Said akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul
Makonda alipotembelea kukagua kiwanda.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiweka jiwe la msingi la
ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Tunduwi Songani.
Wananchi wa Tunduwi Songani wakishuhudia uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi .
Wanafunzi wa shule ya msingi Tunduwi Songani.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akimsikiliza Kaimu Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana kuhusiana na kero wanazozipata
zalugha chafu wanapokwenda katika zahanati .
MKUU
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana hawezi kupandishwa cheo kuwa Mganga
Mkuu wa Wilaya hiyo mpaka hapo atakapotatua changamoto za zahanati ya
Tundu Songani Kata ya Pemba Mnazi.
Makonda
aliyasema hayo mwisho wa ziara yake ya siku ya pili Wilayani Kigamboni
Novemba 20, 2016 wakati alipokwenda kuzindua madarasa ya Shule ya
Msingi Tundu Songani,ambapo mara baada kuzindua madarasa hayo aliongea
na wananchi na kusikiliza kero.
“Kwa
mamlaka uliopewa na Rais wewe ndio mwakilishi wake katika upande wa afya
wilaya ya Kigamboni uwezi kupandisha cheo kuwa Mganga wa Wilaya hii
mpaka hapo utakaponiakikishia kupeleka gari la wagonjwa na kutoa lugha
nzuri kwa wateja”alisema Makonda.
Makonda
alisema awezi kumtumbua jipu Mganga huyo kwa kuwa ameteuliwa muda mfupi
mpaka sasa ana mwezi mmoja hivyo amempa muda kwa ajili ya kumwangalia
katika utendaji wake kama kaimu Mganga mkuu wa Wilaya hiyo.
Hatua
hiyo ya Makonda kutoa agizo la kumchunguza Mganga huyo linafuatia
wananchi wa Tundu Songani kulalamika mbele ya Serikali ya Mkoa kuwa
mganga huyo ajawai kufika eneo hilo na wananchi kupewa lugha chafu
wanapokwenda katika zahanati .
Kwa
upande wake Kaimu Mganga Mkuu huyo,alipoulizwa kuhusiana na malalamiko
ya wananchi alisema yeye kama mganga mkuu anachofahamu changamoto
iliyokuwepo katika zahanati hiyo gari la wagonjwa akuna.
Naye
Mwananchi Asha Abadalah alisema mwanamke Mjamzito akienda katika kituo
hicho anambiwa aende katika hospitali ya Wilaya ya Temeke na Mgaga huyo
ajawai kufika katika Kata hiyo ya Pemba Mnazi ni mara yake ya kwanza.
Wakati
huohuo katika kusogeza huduma za jamii kwa wanachi Makonda alisema
kuhusu kusogeza huduma ya umeme kwa wananchi mradi wa umeme vijijini
utawafikia kila mwananchi atapata umeme huo kwa gharama y ash,27,000 na
kila mmoja atavuta.Alisema utaratibu wa kupata fomu watatangaziwa wote na Watendaji wao wa Mitaa husika
Hivyo wananchi wawe wavumilivu kwa muda wasubilie mradi huo ufike ili wote waweze kupata umeme wa bei raisi .
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wanachi
katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika uwanja wa shule ya msingi
Buyuni ikiwa mwisho wa ziara siku ya pili katika Wilaya ya Kigamboni
jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Buyuni akielezea kero zake.
Wananchi wa Buyuni wakiwa katika mkutano wa hadhara.
No comments:
Post a Comment