Picha na Habari za Freddy Macha, London
Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS) Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose. Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania” Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
Wajumbe wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya. Mama Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu, uongozi mpya wa Rais John Magufuli unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo. Mtanzania na mwanachama wa BTS, Bi. Petronilla Mwakaluma akiuliza swali Balozi Migiro akijadiliana na baadhi ya wataalamu Watanzania waliokuja kumsikiliza. Aliye naye “maso kwa maso” ni mganga shupavu wa kisukari Dk. Gideon Mlawa. Kulia kwake ni mwanafunzi chuo kikuu Wales, Fadhili Maghiya. Mwenyekiti wa BTS, Dk Andrew Coulson akiongoza dimba. Dk Coulson mhadhiri chuo kikuu cha Birmingham aliwahi kufundisha Mlimani Dar es Salaam na kuandika kitabu cha uchumi wa Tanzania miaka ya 70 na 80. Watanzania - Bw Yusufu Kashangwa, Mkurugenzi Kituo cha Biashara London, Mganga Dk Mohammed Hamza Hassan, Mganga Dk Gideon Mlawa, Mwanauchumi Dk Evans Mella na Bi Petronilla Mwakaluma. Bw. Tony Johnson wa Rotary Club akiuliza swali kuhusu maendeleo ya vijiji alivyofanya kazi zamani na anavyoendelea kuvitembela Tanzania. Mheshimiwa Balozi Migiro akizungumza na Watanzania waliohudhuria Waingereza wanachama wa BTS waliofanya kazi Tanzania zamani Mwanafunzi wa chuo kikuu cha SOAS , bi Asha Yussuf na Dk Evans Mella wa Investment Bank, Credit Suisse. Bw Jonathan Pace na wanachama wenzake wa BTSMtanzania Bw Aseri Katanga anayepeleka Kompyuta kusaidia watoto vijijini Nigeria, Zambia, Gambia, Namibia na Tanzania akiuliza swali kuhusu viza zinazowakabali wanaojitolea katika shughuli hiyo.Shirika lake laitwa “Computers 4 Africa.” Balozi Migiro akisogoa na Mwingereza aliyekuwa mwalimu wa shule ya sekondari Minaki, miaka ya 70. Mwanahabari Ben Taylor (gazeti la Tanzania Affairs) akiwa na mpigania haki za Albino, mwanafunzi Ashura Kayupayupa Watanzania - Ashura Kayupayupa, F Macha, Fadhili Maghiya na Asha Yussuf