Afya : Waziri, Ummy Mwalimu azindua mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito , Mtwara na Lindi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Nov 2016

Afya : Waziri, Ummy Mwalimu azindua mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito , Mtwara na Lindi


Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya UJERUMANI, wamezindua mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa Tumaini la Mama. 

Akuzungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amewahimiza wanaume kushiriki kikamilufu kwa kuwapeleka wake zao Kliniki na kupata maelekezo kwa pamoja juu ya matunzo ya ujauzito. 

Aidha amewataka wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuzingatia uzazi wa mpango na kuwapunguza watoto wa kike kwenda shule, badala ya kuwaona mapema

Ummy amesema Mradi huo unalenga kuwahuduma wanawake wanatoka katika kaya masikini ambazo zimekuwa zikilazimika kutumia njia zisizo salama za kujufungua kutokana na kukosa fedha za kugharamia huduma hizo katika vituo vya matibabu. 

Kupitia mradi huo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utawalipia huduma za matibabu wanawake wajawazito wote wa mkoa ya Mtwara na Lindi baada ya kujiandikisha kwenye vituo vya matibabu vilivyosajiliwa karibu nao. 

Mradi wa Tumaini la mama pia utawapa kadi Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wanawake watakaojifungua chini ya mradi huo pamoja na kaya zao. 

Mradi huo ulioanza kutekelezwa ktk mikoa ya Mbeya na Tanga tangu mwaka 2012, umekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa zaidi ya wanawake Laki mbili wamenufaika nao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Aifena Mramba akitoa maelezo mafupi ya Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (katikati) kwa kushirikina na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego (kulia) na Mwakilishi Ubalozi wa Ujerumani,Julia Hannig (kushoto) kukata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi Mayasa Maunda vifaa vya kujifungulia katika uzinduzi wa Tumaini la Mama
Mwimbaji wa muziki wa taarab, Isha Mashauzi akitumbiza kwenye kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Baadhi kina mama waliokabidhiwa vifaa vya kujifungulia wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa Tumaini la Mama
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Baadhi wa viongozi waliogika kwenye uzinduzi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad