Mhe.
Mohammed Haji Hamza, Balozi wa Tanzania nchini Misri akiwakaribisha
wageni waliohudhuria katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya
Tanzania na misri lililofanyika katika miji ya Cairo na Alexandria
kuanzia tarehe 17 hadi 19 Oktoba 2016. Kongamano hili lililowakutanisha
wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili lilifunguliwa na Waziri wa
Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe Balozi Amina Salim Ali.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa na washiriki kutoka sekta mbalimbali zinahusika na
uwekezaji, biashara, ujenzi, usafirishaji, elimu, afya, viwanda,
uhandisi ,kilimo na utalii. Kongano hilo liligharmiwa na kuratibiwa kwa
ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Wizara ya Mambo ya
Nje ya Misri, Jumuiya za Wafanyabiashara wa Misri na makampuni binafsi
ya biashara ya Misri. Katika kongamano hilo washiriki wa Tanzania pamoja
na kutoa mada zilizohusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania
na hasa katika sekta ya viwanda na utalii pia walipata fursa ya
kushiriki katika mazungumzo ya ana kwa ana ya kibiashara.
Siku
ya pili ya kongamano hili washiriki kutoka Tanzania walipata nafasi ya
kutembelea sehemu mbalimbali za uzalishaji na huduma zikiwemo: kijiji
cha teknolojia cha Cairo, viwanda vya utengezaji madawa, vifaa tiba na
rangi za ujenzi mjini Cairo pamoja na viwanda vya nguo, vifaa vya ujezi
na samani za chuma katika miji wa Tenth Ramadhani .
Siku
ya tatu ya kongamano hilo baadhi ya washiriki kutoka Tanzania
walitembelea vyuo vikuu vya Alexandria na chuo kikuu cha kiarabu cha
sayansi, teknolojia na usafiri wa bahari mjini Alexandria na kuwa na
mazungumzo ya ushirikiano na viongozi wa vyuo vikuu hivyo.
Ujumbe
wa Tanzania pia ulipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha kutengenezea
manukato kilichopo nje kidogo ya jiji la Akexandria. Akiwa jijini Cairo,
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo alipata nafasi ya
kukutana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Rais na Mtendaji
Mkuu wa Afri exim bank na Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na
Maendeleo wa Misri.
Vingozi
mbalimbali walioshiriki kwenye ufunguzi wa konganano la kibiashara
mjini Cairo siku ya tarehe 17 Oktoba 2016 wakisimama wakati wa Nyimbo za
Taifa za Tanzania na Misri zilipopigwa. Wa kwanza kutokea kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Misri. Wa pili ni
Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na Maendeleo wa Misri, watatu ni
Mhe Balozi Amina Salim Ali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa
Zanzibar, akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Mohamed
Haji Hamza , watano ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,
Zanzibar na wa sita ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Biashara
ya Misri. Waliosimama mbele ya meza kuu ni Mabalozi kutoka nchi za SADC
waliopo mjini Cairo.
Balozi
Amina Salum Ali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar
akifuatilia neno la ukaribisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini
Misri, Mhe. Mohammed Haji Hamza .
Balozi
Hamza akisalimiana na kubadilishana mawazo na washiriki mbalimbali wa
kongamano la biashara jijini Cairo mara baada ya ufunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment