Katika
kusaidia kuboresha elimu nchini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesaini mikataba miwili na serikali
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyo na lengo la
kusaidia elimu nchini.
Mkataba
wa kwanza unahusu mradi unaofahamika kama 'Empowering Adolescent Girls
and Young Woman through Education' mradi ambao umedhaminiwa na Shirika
la Misaada la Korea (KOICA) kwa kiasi cha pesa cha Dola Milioni tano
(5,000,000), mradi ambao unataraji kufanyika katika wilaya ya
Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Micheweni, Pemba.
Mkataba
wa pili unahusu mradi wa 'XPRIZE - Promotion of Early Learning Through
the use of Innovative Technologies' ambao umedhaminiwa na UNESCO kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula (WFP) kwa kiasi
cha pesa cha Dola Milioni mbili (2,000,000) ambapo utahusisha watu wa
miaka 15-18 ambao hawapo shuleni kutoka Arusha na Tanga ambapo
watapatiwa tablet ambazo zitakuwa na programu tumishi za kujifunza.
Akizungumza
wakati wa kusaini mikataba hiyo, Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO,
Zulmira Rodrigues alisema mipango ya UNESCO ni kuona inawasaidia watoto
ambao hawasomi licha ya kuwa na umri wa kuwa shuleni wakipata nafasi ya
kusoma ili kupunguza idadi ya watoto ambao hawapo shuleni duniani
ambapo takwimu zinaonyesha wanazidi Milioni 263.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akizungumza kuhusu mradi wa Empowering Adolescent Girls and Young Woman
through Education na XPRIZE - Promotion of Early Learning Through the
use of Innovative Technologies.
"Tunaandika
histori leo sio kwa Tanzania bali dunia nzima, maana makubaliano
yataleta ushirikiano kati ya WFP, UNESCO na Wizara ya Elimu kuwasaidia
watoto zaidi ya Milioni 263 ambao hawapo shuleni duniani na kutumia
nafasi ya teknolojia kutafuta suluhisho la kuwasaidia watoto hawa,
"Tunaishukuru
Wizara ya Elimu kwa kutuamini, nawashukuru WFP kwa kuwa pamoja nasi na
kwa washirika wengine ambao wamekubali kuungana nasi kwa ajili ya
kufanikisha hili," alisema Rodrigues.
Nae
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish
alisema msaada huo utaweza kusaidia kuboresha elimu nchini hasa katika
kipindi hiki ambacho serikali inajipanga kutoa elimu kisasa kwa kutumia
njia za kidigitali na hivyo ni mwanzo mzuri kwa mfumo ambao wanajipanga
kuanza kuutumia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish akitoa neno la shukrani kwa niaba ya serikali.
"Kwa
niaba ya serikali ya Tanzania tunashukuru kwa msaada wenu kwa kuwa
tayari kusaidia elimu ya Tanzania kwa kutumia teknolojia, tunataka kutoa
elimu kwa njia ya kidigitali na nyie mmekuwa tayari kutusaidia
tunawashukuru,
"Madhumuni
makubwa ni kutaka kuboresha elimu na tukaona ni vyema kushirikiana na
mashirika mengine ili kuwasiadia watoto kupata elimu bora kwa kufuata
zile njia tatu, Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, shuleni atafundishwa na
akirudi nyumbani anaweza jifunza kusoma kwa kutumia tablet," alisema
Kwa
upande wa Mwakilishi wa WFP nchini, Michael Dunford alisema WFP imekuwa
ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali hivyo
kuwa sehemu ya kusaidia elimu nchini ni jambo kubwa na lengo lao ni
kuona teknolojia inakuwa na faida kusaidia elimu kukua.
Mwakilishi
wa WFP nchini, Michael Dunford akielezea jinsi WFP imeguswa hata
kufikia hatua ya kuwa tayari kushirikiana na UNESCO kufanya mradi wa
XPRIZE.
"WFP na
Wizara ya Elimu wamekuwa wakishirikina kwa muda mrefu na hata UNESCO
tunataka kutumia teknoloji kusaidia elimu, kuona jinsi gani teknoloji
itatumika madarasani na WFP tayari ina watu ambao watasimamia
kuhakikisha jambo hili linafanikiwa," alisema Dunford.
Nae
Mkurugenzi wa KOICA nchini, Joonsung Park alisema mradi huo ni sehemu ya
miradi ambayo KOICA imepanga kuifanya kwa ajili ya kusaidia kukuza
elimu katika nchi ambazo zinaendelea.
Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akieleza jinsi miradi hiyo itakavyofanya kazi.
Mkurugenzi
wa KOICA nchini, Joonsung Park akizungumza kuhusu mradi ambao
wamedhamini ambao pamoja na una lengo la kusaidia elimu na zaidi kwa
wasichana.
"Huu ni
moja ya miradi mitatu ambayo KOICA imekubaliana na UN kwa ajili ya
kuifanya na kusaidia elimu, tumekuwa tukishirikiana na UNFPA, UNWOMAN,
UNV katika kufanikisha hilo na matarajio yetu ni kuwa ushirikiano wetu
uzidi kudumu na kuleta matokeo mazuri," alisema Park.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish
wakisaini mkataba wa mradi wa XPRIZE.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish
wakisaini mkataba wa mradi wa Empowering Adolescent Girls and Young
Woman through Education.
No comments:
Post a Comment