Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera
ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini
kwake jijini Dar salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera
ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo
leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifurahia Zawadi ya
Tai ya Bendera ya Taifa aliyopewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,
Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali kitabu cha Sheria kuhusu matumizi ya Vielelezo
vya Taifa kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika
Mashariki.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na
Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa Bendera ya
Taifa na ile ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,
Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.
Na Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara,
Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa
kama bendera na nembo ya taifa katika ofisi zao ili kuenzi tunu na
vielelezo vya Taifa.
Aliyasema
hayo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa
akipokea rasmi bendera ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo.
Alisema kuwa vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.
“Sheria
pia inavitambua vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake,
kwani hata mtu akichezea vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya
sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.
Aliongeza
pia Mahakama ya Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake
kama ilivyo kwa Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili
ziweze kutumika katika Mahakam azote nchini.
Awali;
akiongea na Jaji Mkuu pamoja na waandishi wa habari kabla ya
makabidhiano hayo, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo
pia alizitaka Taasisi za Serikali kutopuuzia umuhimu wa matumizi wa
vielelezo vya Taifa.
Alisema
kuwa baadhi ya Ofisi nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo
vingine muhimu ambavyo vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake
ili kuenzi tunu za Taifa.
“Ofisi
nyingi za Serikali zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina
kabisa, vitu hivi ni muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na
kuvithamini pamoja na kuvitunza,” alisema Bw. Chibogoyo.
No comments:
Post a Comment