Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce
Msiru wakati alipowasili katika chanzo cha maji cha Shiri kwa ajili ya
zoezi la kuotesha miti ikiwa ni kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa
Taifa ,Hayati Mwl Julius Nyerere.
Wakuu
wa wilaya za Hai na Moshi ,Gelasius Byakanwa (wa pili toka kulia) na
Kippi Warioba (wa tatu toka kushoto waliungana na Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro katika zoezi hilo.kulia ni Katibu tawala wa mkoa wa
Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la uoteshaji miti.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiotesha mti katika eneo la
chanzo cha maji la Shiri Njoro lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akiotesha mti katika eneo hilo zoezi
ambali lilishirikisha watumishi wa idara mbalimbali za serikali na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Majsafi na Usafi wa Mazingira mjini
Moshi(MUWSA).
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika eneo hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na viongozi wa
wilaya pamoja na wananchi wengine kutembelea chanzo cha maji cha Shiri
Njoro .
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Moshi
Kippi Warioba (anayefuatia pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
wakitizama eneo ambalo kunafanyika mgawanyo wa maji katika chanzo cha
maji cha Shiri Njoro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment