Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akihutubia wakati alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipokuwa amewasili kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam jana. Kushoto ni mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila. Manyanya alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto niMwanasiasa Wilson Mkama akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Mwenyekiti wa kongamano hilo, Spika wa Bunge mstaafu, Anna Makinda akizungumza kwenye kongamano hilo.
wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila, akizungumza kwenye kongamano hilo. Kongamano hilo liliandaliwa na chuo hicho.
Waalikwa wakisikiliza wakati mada zikiendelea kutolewa.
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philipo Mangula,amesema ameanza kupokea mafaili ya wana CCM ambao wameanza kujipitisha kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho unaotajariwa kufanyika mapema mwakani.
Mangula amesema ana taarifa kwamba wanaCCM wengi wameanza kutumia mbinu chafu za fedha kutaka nafasi mbalimbali na kwamba imekulakwao kwakuwa hawataweza kupenya atawashughulikia.
Mangula alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mada ya maadili ya viongozi kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam jana na kueleza kukerwa na tabiya ya wafanyabishara wenye fedha ya kutaka kuteka kila mahali.
Alisema ndani ya CCM nimaarufu kwa jina la mzee wamafaili, hivyo ataendelea kupitia mafaili hayo ilikuhakikisha maadili yanazingatiwa na kuenzi misingi yaAzimio la Arusha kwani hakuna atakayepenya kwa njia za rushwa.
“Zipo taarifa kuwa wapo baadhi wameanza kujipitisha na kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani, nawahakikishia kwangu watu hao hawawezi kupitani tamfuatilia kila mmoja atakaye jihusisha na rushwa hapati nafasi hiyo,” alisema.
Alisema ili kudhibiti mianya hiyo atahakikisha sheria inatungwa ya kutenganisha kati ya wafanyabiashara na uongozi kwa vile wafanyabishara wanatafuta nafasi ya uongozi ilikuendeleza biashara zao.
Mangula alisema ni aibu kwa mpiga kura kuhongwa kiasi kidogo cha pesa na kupoteza haki ya msingi ya kumchangua kiongozi mwenye sifa kwa ajili ya maendeleo.
Alisema iwapo tabia ya kununua uongozi itaendelea baadaye vijana wanaohitimu masomo watakosa nafasi ya kugombea uongozi kutokanana kukosa pesa za kuhonga.
Watanzania wanapaswa kufahamu hatua zinazochukuliwa naRais John Magufuli kuwatumbua watumishi wazembe, imetokana na kauli ya vikao halali vya CCM ili atekeleze hayo.
“Huo ni mpango mkakati wa chama kwa lengo la kuondokana na rushwa, vinginevyo misingi na maadili ya uongozi itapotea,” alisema.
Spika mstaafu na Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Anna Makinda amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwapeleka vijana wao katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere (MNMA) kujifunzasomo la maadili ya kiongozi ili kuepuka rushwa.
Alisema kongamano hilo limezingatia mada kuu tatu ambaoni Azimio la Arusha, miiko ya uongozi na maadili ya viongozi ambayo kiongozi anapaswa kujitathimini.
Mmoja wawatoa mada, Wilson Mkama alisema viongozi wengi wasiasawapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi kupata utajiri, ikiwamo nyumba, gari nafedha.
Hali hiyo inawafanya watumiegharama yoyote kupata nafasi ya uongozi huku akijua fedha hizo alizotoa zitarudi na kutengeneza maisha mapya.
“Wapo viongozi kwa ajili ya maslahi yao na siyo kwa maslahi ya jamii, huko nikutoka nje ya maadili,” alisema.
No comments:
Post a Comment