Burudani : Vijana nchini washauriwa kujiajiri kupitia Sanaa - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Oct 2016

Burudani : Vijana nchini washauriwa kujiajiri kupitia Sanaa


Katika kukabiliana na upungufu wa ajira hapa nchini Vijana wameshauriwa  kujiajiri  kupitia Sanaa na vipaji walivonavyo katika kupata kipato.

Ushauri huo umetolewa Wilayani  Bagamoyo na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi alipokuwa anawahutubia wahitimu wa Astashahada na Stashahada  ya Sanaa na Ufundi katika Chuo cha Sanaa na Ufundi  Bagamoyo  kilichopo  chini ya Taasisi ya Sanaa  na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

“Tumieni elimu mliyopata   kujiajiri wenyewe ili kuepuka changamoto ya ajira iliyopo hapa  nchini, ujuzi mliopata  ni njia pekee ya kujiletea kipato na Taifa kwa ujumla”.Alisema  Bibi Leah.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa  wasanii wote wanaofanya kazi za Sanaa ni vyema wakasajili  kazi zao katika Mamlaka husika  ili iwe rahisi kwa Serikali  kutoa msaada kwa urahisi kwaWasanii hao.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu waTaasisi ya Sanaa na Utmaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbet  Makoye aliwasihi  wahitimu hao kuwa mabalozi  wazuri wa sanaa  watakapokuwa wanafanya shughuli zao za Sanaa.

“Nendeni mkawe mabalozi  wazuri wa Chuo  chetu kwa kuwa Wasanii  bora na kutengeneza  kazi nzuri ili muweze kushindana  na soko la ajira”. Alisisitiza Dkt.Makoye.
Naye mhitimu wa ngazi ya  Stashahada ya Sanaa na  Ufundi  Bi Imelda John amesema  kuwa elimu aliyoipata itamsaidia  kufanya kazi ya Sanaa kwa weledi zaidi hasa katika  fani ya kutengeneza Filamu na Picha Jongefu.

Mahafali hayo ni ya 27 katika chuo hicho ambapo kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 85 wametimu Astashahada na Stashahada ya Sanaa na Ufundi. imeandikwa na Shamimu Nyaki- WHUSM.
aimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi akizungumza na wahitimu pamoja na wageni mbalimbali (hawapo pichani) katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt.Herbet Makoye akisoma hotuba kwa Mgeni Rasmi pamoja na wageni mbalimbali (hawapo pichani) katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.

Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (wa tatu kulia) akiwatunuku vyeti vya kuhitimu Stashahada ya Sanaa na Ufundi baadhi ya wahitimu ) katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.
Wanachuo wa Chuo cha Sanaa na Ufundi Bagamoyo wakicheza ngoma katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.
Wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Sanaana Ufundi Bagamoyo wakicheza kwaya katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) pamoja na wahitimu wa ngazi ya Astashaha katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi hiyo .Wa kwanza Kulia Mkuu wa Idara ya Elimu ya Taasisi hiyo na Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt.Herbet Makoye.
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) pamoja na wahitimu wa ngazi ya Stashaha katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi hiyo .Wa kwanza Kulia Mkuu wa Idara ya Elimu ya Taasisi hiyo na Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt.Herbet Makoye.


Vikundi mbalimbali vya burudani kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) vikitoa burudani kwa wananchi pamoja na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) katika ufungaji wa Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi hiyo Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi akiangalia bidhaa za urembo kutoka kwa mbunifu Mariam Kiiza kabla ya kufunga Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Baadhi ya wanachi walioshiriki ufungaji wa Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.

Post Top Ad