Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Wafanyabiashara
wa maduka yaliyoko katika eneo la Stendi Ndogo jijini Arusha wameandamana
katika Ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wakidai mikataba ya kupangisha
katika maduka hayo yanayomilikiwa na Halmashauri kufuatia mgogoro kati yao na
Wajenzi wa maduka hayo.
Kutokana na
Sintofahamu hiyo wamelazimika kuandamana nje ya Ofisi za Halmashauri
wakishinikiza kupewa mikataba ya upangaji na kudai kuwa wamechoshwa na vitisho
wanavyovipata kutoka kwa wajenzi wa maduka hayo ile hali wanalipa kodi kwa
Halmashauri.
Prisca Lema na Witness Riwa ni Wafanyabiashara katika
soko hilo wamesema kuwa licha ya kupewa barua rasmi za kutambulika kama
wapangaji wa Halmashauri bado hawajapewa mikataba suala linalowaweka njia panda
na kutokujua hatma yao na kunahatarisha
mitaji yao pamoja na mikopo waliyoichukua katika taasisi za fedha.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara Hao Josephine Exuper amesema kuwa licha ya tume iliyoundwa
na Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo
kutokukamilisha kazi yake na kutoa muafaka tayari wajenzi hao wameanza
kujichukulia hatua mikononi na kuwatishia kuwafukuza katika maduka hayo na
kudai kuwa wao ni wamiliki halali na si halmashauri.
Meya wa Jiji
la Arusha Kalisti Lazaro amesema kuwa Baraza la Madiwani tayari limeridhia wapangaji
hao kupewa mikataba na Ofisi yake imeweka saini sahihi pekee iliyosalia ili
mikataba hiyo iwe tayari ni ya Mkurugenzi wa Jiji kwani uamuzi huo unaungana na
Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG wa kutaka kuondoa madalali katika
upangishaji wa majengo ya serikali ambao unapelekea kupoteza Bilioni 2.1 ya mapato ya serikali.
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha hakupatikana katika Ofisi yake kwa kuwa alikua nje ya Ofisi
akitimiza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment