Matukio : DC Muheza apiga Marufuku Bodaboda kuendeshwa zaidi ya Saa sita - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Sept 2016

Matukio : DC Muheza apiga Marufuku Bodaboda kuendeshwa zaidi ya Saa sita



Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.





Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.

Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya hiyo,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo,Ally Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza(DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.



Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza,Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili


Baadhi ya waendesha bodaboda wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza nao kusisitiza umuhimu wa wao kutii sheria za usalama barabarani ikiwemo kuacha kufanya vitendo vya uhalifu


 Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimepaki kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad